Habari za Punde

Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Aipa Tano Foutain Gate

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa pongezi kwa Shule ya Fountain Gate kwa kuendelea kuwekeza katika michezo ambayo imeifanya shule hiyo iwe miongoni mwa Shule zinazoiletea heshima Tanzania.
Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa pongezi kwa Shule ya Fountain Gate kwa kuendelea kuwekeza katika michezo ambayo imeifanya shule hiyo iwe miongoni mwa Shule zinazoiletea heshima Tanzania.
Mhe. Mwinjuma ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya Usiku wa Tuzo za Wanamichezo iliyoandaliwa na Shule hiyo, Mei 20,2023 jijini Dodoma akieleza kuwa kuwa Serikali inaendelea kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali wanaoendeleza na kuwekeza kwenye Sekta ya Michezo.
"Natoa pongezi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa namna linavyouosimamia mpira wa miguu nchini, natoa wito liendelee kufanya hivyo na kuongeza juhudi katika kupinga rushwa michezoni. Na katika kipindi cha likizo ni vyema wanamichezo wakaendelea kufanya mazoezi pamoja na kutunza miili yao" amesisitiza Mhe. Mwinjuma.
Awali Mkurugenzi wa Fountain Gate Sports Academy Bw. Japheth Makau amesema lengo la Tuzo hizo ni kuthamini mchango wa wanamichezo wa shule hiyo ambao wameiletea heshima Tanzania pamoja na shule hiyo ndani na nje ya nchi.
Ameeleza kuwa mpaka sasa Shule hiyo inashikilia ubingwa wa Afrika kwa Shule za Sekondari, Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya miaka 15, huku ikiwa na wachezaji 11 katika timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa miguu pamoja na wachezaji wawili wa kulipwa katika nchi ya Uturuki na Misri.
Tuzo zilizotolewa na pamoja na  Mchezaji Bora Chipukizi iliyoenda kwae Mariam Semgomba, Mshambuliaji Bora Frida Gerald , Mchezaji Bora Monica Chebel na nyingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.