Habari za Punde

Mtanzania Vick Elias Aobika Mshindi wa Mashindano ya Gofu Nchini Kenya

 


Na. Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa pongezi kwa Mtanzania Bi. Vick Elias kwa kuibuka wa kwanza katika mashindano ya Gofu ya Muthaiga Ladies Open 2023 yaliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya.

Mhe. Chana ametoa pongezi hizo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifunga  Mashindano ya Gofu ya Lugalo Ladies Open 2023, ambapo  ametoa Rai kwa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali hususani mchezo wa Gofu kwa kuwa katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira.

"Nalipongeza JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi kutumia Klabu hii katika kuendeleza vipaji vyao na kukuza mchezo wa Gofu ambao unaendelea kukua siku hadi siku" amesema Mhe. Chana.

Awali Mwenyekiti wa Lugalo Gofu Club Brigedia  Jenerali  Mstaafu, Michael Luwongo  amesema mashindano hayo yameshirikisha wanamichezo takriban 100 ambapo Wanawake ni zaidi ya 50.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.