Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Akiendelea na Ziara Yake Nchini Qatar Akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi alihudhuria dhifa ya chakula cha mchana iliyokuwa imeandaliwa na Mfanyabiashara maarufu kutoka Qatar Feisal Bin Qassim Bin Feisal Bin Thani Bin Qassim Bin Mohamed Al Thani. Mfanyabiashara huyu ni mmiliki wa hoteli 30 kubwa duniani na makumbusho ambayo yana vitu vingi vya kusisimua vya zamani.

Baada ya dhifa ya chakula cha mchana, Rais Dk Hussein Ali Mwinyi, pamoja na Mama Mariam Mwinyi na ujumbe wake, walipata fursa ya kutembezwa ndani ya makumbusho hayo, Makumbusho hayo yana mkusanyiko mkubwa wa vitu vya kihistoria kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Moja kati ya vitu vilivyomvutia Rais Mwinyi ni noti ya zamani ya Zanzibar iliyotumika mwanzoni mwa mwaka 1916. Kupata noti hiyo katika makumbusho ya nchi ya Qatar kunadhihirisha ushawishi na utajiri wa historia ya Zanzibar na thamani yake katika historia ya dunia.

Mbali na noti hiyo, makumbusho hayo pia yanahifadhi aina mbalimbali za magari ya zamani, yakiwemo yale yaliyotengenezwa mnamo mwaka 1890.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.