22 Julai, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi amesema suala la msaada wa
kisheria sio la Zanzibar pekee, bali ni la kimataifa, lina historia kubwa duniani.
Alisema, Zanzibar
ina wajibu wa kutekeleza kwa vitendo huduma za sheria kama lilivyoelezwa kwenye
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 12 pamoja na Sheria nyengine
mbalimbali zilizopo nchini.
Rais Dk. Mwinyi
aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa
Sheria, yaliyofanyika ukumbi wa Idrissa Abdul wakili, Kikwajuni Wilaya ya
Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, watoaji
wa msaada wa sheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa
wananchi wasio na uwezo wa fedha katika msada wa sheria.
Dk. Mwinyi
alieleza lengo la kilele cha maadhimisho hayo ni kuzifanya huduma za kisheria kuwa
endelevu na zenye kuleta tija kwa jamii sambamba na kutatua changamoto nyengine
zinazokwaza huduma za utoaji wa kisheria nchini.
Alieleza Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na
Utawala Bora itaendelea kushirikiana na watoa msaada wa kisheria kwa
kuhakikisha wanaendelea kutwaa tunzo zaidi, pia wanapata mazingira bora ya
kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Pia Dk. Mwinyi
alieleza Serikali itahakikisha marekebisho ya Sera na Sheria ya Msaada wa
Kisheria yanafanyika kwa ufanisi na haraka ili kukidhi matakwa yanayotakiwa.
Akizungumzia suala la
upatikanaji wa vifaa na vitendelea kazi kwa wasaidizi wa wasaidizi wa kutoa
msaada wa sheria, Rais Dk. Mwinyi aliwaahidi
kwamba seikali inaungamkono shughuli wanazozifanya b
upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi nayo ni changamoto nyengine. Mazingira wezeshi ya utoaji huduma yanahitaji kuwa na vifaa vya kutosheleza, vikiwemo vyombo vya usafiri, vifaa vya Ofisi kama vile printa, mashine za Fotokopi, Komputa na kadhalika. Vinapokosekana vifaa hivi, ni dhahiri kuwa daraja la ufikiaji haki nalo hukosekana.
Aidha, aliwataka
watendaji mbalimbali wa Serikali na taasisi binafsi na vyombo vya kusimamia
haki, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Watoaji msaada wa kisheria ili
kuwajengea uwezo wa kufanikisha kazi zao kwa uweledi. Sambamba na kuwaunga
mkono na kupata ushirikiano wa kutosha.
Hata hivyo alitoa kwa
jamii nakuwataka kutimiza wajibu wao kila mmoja kwanafasi yake ili kuwe na mazingira
bora ya upatikanaji msaada wa kisheria na kuzidi kuimarisha kiwango cha utawala
bora nchini na misingi ya haki za binadamu.
Akizungumza kwenye hafla
hiyo, Jaji Mstafu Robert Makaramba alisema, maadhimisho ya 2023 yamekwenda
sambmba na mazingira ya uboreshaji wa
mifumo, miundo, sera na sheria zinazohakikisha huduma za msaada wa sheria
zinatolewa katika hadhi ya zenye lengo la kufikia uwezeshaji wa Serikali kwa
kushirikiana na watoa msaada ya kisheria, wadau wa maendeleo, taasisi za
kiraia, wadau wa sekta za haki wakiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Polisi, Chuo cha Mafunzo na jamii husika.
Nae Mkurugenzi wa Idara
ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Hanifa Ramadhan Said alieleza, watoaji wa msaada wa sheria wanafanya kazi kwa kujitolea na uzalendo kwa uhakikisha
wananchi wa Zanzibar wasio na uwezo wanafikiwa na huduma za
kisheria kwa sehemu zote ili kutatuliwa haja zao kisheria.
Alisema, maadhimisho
hayo walishirikiana na taasisi zote zinazohusu masuala ya sheria, wakiwemo
Mahakama, jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu, Chuo cha Mafunzo na wadau wengine.
Maadhimisho hayo ya
msaada wa sheria yaliyokuwa na kauli mbiu “Mazingira wezeshi kwa watoa
msaada wa kisheria ni daraja la upatikanaji haki” ambayo yalianza Julai 17 na kuadhimishwa Julai 22 mwaka
huu yalitanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji ikiwemo kampeni ya
vyumbo vya Habari, mkutano na vyombo vya Habari, kutembelea vyombo 21 vya
Habari, kufanya program ya vijana kwa Unguja na Pemba, mihadhara na jamii,
kufanya usafi wa mazingira kwenye hospitali ya wagonjwa wa Akili,
Kidongochekundu, kufanya bonaza na hatimae kuadhimisha kilele halisi wiki ya
msaada wa kisheria.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment