Habari za Punde

Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto kushirikiana na wadau wa maendeleo

 Na Maulid Yussuf WMJJWW 


Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi Siti Abbas Ali amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuona yale yote yaliyopangwa. Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto bi Siti Abbas Ali amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuona yale yote yaliyopangwa yanafikiwa.

Mkuu wa Divisheni ya Jinsia katika Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto ndugu Ali Wadi ameyasema hayo  kwa niaba yake wakati alipofunga mafunzo kwa Waratibu wa wanawake na watoto wa Shehia, kwa Wilaya za Magharibi B' katika ukumbi wa Kituo cha Walimu TC Kiembesamaki Mjini Unguja.

Amesema hivi sasa Wizara inaendelea katika mapitio ya sheria ya mtoto no. 6 ya mwaka 2011,  ili kuona inakidhi mahitaji  kwa kushirikiana na Kijiji cha SOS. 

Aidha ameiopongeza SOS kwa kuona umuhimu wa kuingia programu zake kwa Waratibu na  kusaidia katika changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuwarahisishia katika utendaji wa kazi zao.

Amesema amewaahidi kuwa changamoto walizozielezea Wizara inazitambua na inaendelea kuzipatia  ufumbuzi.

Hata hivyo amewaomba kuzidisha mashirikiano baina yao na wadau wa Maendeleo pamoja na wizara ili kusaidia kupunguza tatizo la udhalilishaji nchini.

Naye Mratibu wa Programu wa bi Nyezuma Simai Issa ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa mashirikiano wanayotoa  kwa kijiji cha SOS katika kuhakiksisha wanafanikisha kazi zao.

Amesema kijiji cha SOS Zanzibar kimedhamiria kuona kuwa Maendeleo ya watoto yanakuwa pamoja na ustawi wao kwa kuona kila mtoto wa kizanzibari anakuwa na malezi bora na imara na wanapata haki zao zote kama inavyostahiki.

Amesema miaka 20 nyuma Kijiji cha SOS pamoja na harakati zake, hivi sasa imeona ni muhimu kufanya kazi na waratibu wa wanawake na watoto Kimikoa na kusikiliza changamoto zao katika kuona wanafanyakazi vizuri katika kuwasimamia watoto.

Aidha amesema wataendelea kuwashajiisha wafadhili wao  kuendelea kusaidia kwa kuongeza nguvu katika miradi mbalimbali ya watoto ili kufikia malengo.

Mapema Waratibu wa Wilaya za Magharibi B,  wamesema wanachangamoto mbalimbali ikiwemo  upatikanaji wa posho zao kwani wameshafungua akaunti za benki mwaka mmoja sasa lakini bado hawajaingiziwa.

Wamesema pia bado wanatatizo la kutokuwa na vitambulisho jambo ambalo linawapa ugumu katika utendaji wao wa kazi yanafikiwa.

Kijiji cha SOS kinaendelea na utaratibu wa kuwakutanisha waratibu wa wanawake na watoto katika shehia kupitia Wilaya mbalimbali ili ujua changamoto zinazowakabili katika kazi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.