Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Ameongaza Wanananchi Katika Maziko ya Amiri Mkuu wa Markazi ya Fuoni Ijitimai Amiri Sheikh.Wakati Hassan Wakati

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Markaz Kuu ya Fuoni Ijitimai Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-7-2023,alipowasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuhudhuria maziko ya Amiri Mkuu wa Markazi Fuoni Ijitimai Wakati Hassan Wakati

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kubeba jeneza na Waumini wa Dini ya Kiislam kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Maiti ya Amiri Mkuu wa Markazi ya Fuoni Amiri Wakati Hassan Wakati, iliyofanyika katika masikiti huo leo 20-7-2023 na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika kuitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti ya Amiri Mkuu Wakati Hassan Wakati, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Markaz Fuoni Ijitimai Zanzibar leo 20-7-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Alhajj Mhe. Haroun Ali Suleiman na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi na (kulia kwa Rais) Katibu wa Idara ya Uenezi na Itikadi CCM Zanzibar Alhajj Khamis Mbeto na Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe. Abass Mwinyi.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Amiri Mkuu wa Markazi ya Fuoni Ijitimai Amiri Wakati Hassan Wakati, maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-7-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa Pole kwa Mtoto wa Marehemu Amiri Wakati Hassan Wakati. Hassan Wakati Hassan, baada ya kumalizaka kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-7-2023


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.