Habari za Punde

Wanawake na Vijana Wahimizwa Kutumia Fedha za Mikopo katika Makusudio

Afisa mwezeshaji vikundi vya hisa  katika mradi wa viungo  Lalo Kukas akizungumza na mkulima wa mbogamboga na matunda Mpaji Khamis Haji kuhsiana na matumiza ya fedha wanazokopa katika hisa zao wakati mwezeshaji huyo alipomtembelea kuangalia maendeleo ya kilimo chake huko Mgambo Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja
Afisa mwezeshaji vikundi vya hisa  katika mradi wa viungo  Lalo Kukas akikagua shamba la Mkulima Fumu  Mcha Fumu wakati wa ziara yao ya kutembelea mashamba ya wakulima kukagua matumizi ya fedha wanazokopa katika vikundi vya hisa  kwaajili ya kilimo huko Mfenesini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja 
PICHA NA FAUZIA MUSSA - MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahma Khamis Maelezo
Afisa Muwezeshaji ambae pia ni Msimamizi Vikundi vya kuweka na kukopa Agness Nicodemus amewataka wanawake na Vijana wanaochukua mikopo kuelekeza nguvu zao katika kuendeleza kilimo ili kuzalisha zaidi na  kujiongezea kipato.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya kilimo kwa wanavikundi vya kuweka na kukopa iliyofanyika maeneo mbalimbli ya Unguja
Amesema wanavikundi wengi wanaochukua mikopo hawafikii malengo ya uzalishaji kutokana na kutoweka mikakati madhubuti juu ya mikopo hiyo ambayo itawasaidia kuboresha kilimo  na  kujiletea maendeleo, hivyo amewataka wanavikundi hao kujiwekea malengo ya muda mrefu ili kufikia malengo ya mikopo hiyo.

Amefahamisha kuwa lengo la ziara hiyo ni kuona matumizi ya fedha wanazokopa katika hisa zao zinatumika katika malengo yaliokusudiwa na kwa namna gani mradi umewanufaisha .

“Tunataka tujue unachukua mkopo unafanyia kitu gani unawekeza katika kilimo , biashra au maendeleo ya kifamilia  tufikie mahali vikundi viwe vinajitegemea wenyewe katika kujiongezea hisa,”alifafanua Afisa Muwezeshaji

Aidha amewataka wanavikundi hao kuwa na nidhamu ya fedha katika matumizi kwani  endapo hawatozitumia ipasavyo watakosa kujiletea maendeleo jambo ambalo litarejesha nyuma jitihada za Mradi wa Viungo katika kuwasaida wanawake na vijana waliowengi.

Katika hatua nyengine Afisa huyo ameeleza kuwa madhumuni ya kutoa mafunzo hayo ni kununua hisa, kuekeza na kusaidiana katika uwekezaji wa shuhuli zao za kila siku.

Afisa Muwezeshaji amefafanua kuwa katika ziara hiyo  wamewatembelea wale ambao wamepatiwa mafunzo ya hisa  na wanaendelea na utowaji wa mafunzo hayo kwa wanavikundi 67 huku wakiwa katika maandalizi ya  kupatiwa ruzuku wale ambao wamefanya vizuri katika kutumia mikopo ya hisa zao.

Nae Mkulima wa mazao ya matango,matikiti  na mihindi Mpaji Khamis Haji amewashauri wanawake wenziwe kuacha kujiacha na kutegemea wanaume na badala yake kujikita katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi.

Aidha amefahamisha kuwa elimu aliyopatiwa kutoka Mradi wa Viungo juu ya matumizi bora ya mbegu pamoja na dawa za asili katika mimea kumememsdia kwa kiasi kikubwa kwani ameweza kulima na kupata mavuno mengi.

“Elimu ya hisa niliyopatiwa kutoka Mradi wa Viungo kuhusu matumizi bora ya mikopo katika vikundi imeniwezesha kuweza kulima mazao yangu kwa wingi na kupatiwa mkopo katika kikundi changu nashkuru nimefanikiwa vya kutosha kwani nimewza kujenga nyumba yangu mwenyewe,”alieleza Mkulima.

Katika Ziara hiyo maafisa wa mradi wa viungo shirika la PDF waliwatembelea wakulima mbali mbali katika mashamba yao ikiwemo Mfenesini,Chaani na Mgambo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.