Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira amewataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya utekelezaji wa miradi ya mazingira iliyopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuzuia uharibifu wa mazingira na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Jafo
ameyasema hayo Julai 12, 2023 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua
maendeleo ya mradi tuta kupitia Mradi wa kuongeza uhimili wa mabadiliko ya tabianchi
unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika Shehia ya kiongoni
bonde la mto tovuni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar.
Kwa mujibu wa
Jafo amesema athari za mabadiliko ya tabianchi kwa sasa zimeanza kujionyesha
katika baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akitolea mfano
Wilaya za Longido, Simanjiro na Kiteto ambapo dalili za wazi zimejionesha kwa
mifugo kupoteza maisha kutokana na hali ya ukame.
“Kule Bara kwa
sasa ukienda Wilaya za Longido, Simanjiro na Kiteto wafugaji wengi mifugo yao
inakufa kwa sababu hakuna maji wala hakuna malisho na mito mingine imekauka
maji na mfano mzuri ni Mto wa Ruaha Mkuu ambao uliopoteza uwezo wa kutitirisha
maji kwa muda wa siku 100” amesema Waziri Jafo.
Akifafanua
zaidi, amesema kuwa kutokana na ukubwa wa athari za mabadiliko ya tabia nchi
pia baadhi ya maeneo ya Zanzibar ikiwemo kisiwa cha Pemba pia kumeanza
kujionesha kwa dalili mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari
hatua inayosabisha maji ya bahari kuingia katika maeneo ya wananchi.
Kutokana na
changamoto hiyo, Waziri Jafo aliwataka wananchi wa Sheia ya Tovuni kulinda
miundombinu ya ujenzi wa mradi unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais Zanzibar kutokana na eneo kuwa ni miongoni yaliyopo katika hatari kubwa ya
kumezwa na maji ya bahari.
“Maji haya ya
bahari yakiingia katika mashamba yanasababisha mkulima aliyezoea kulima mazao
ashindwe kuendelea na kilimo ikaonekana maeneo mengine ni lazima yawekwe
matuta. Ofisi yangu kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar tulifanya ziara ya miradi mbalimbali ya TASAF ili kujionea maeneo yote
yanahitaji ujenzi wa matuta ili kuzuia maji ya bahari kuingia katika mashamba”
amesema Dkt. Jafo.
Kwa mujibu wa
Dkt. Jafo amesema ameamua kutembelea mradi huo wa kuhimili mabadiliko ya tabia
nchi unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kutokana na historia ya
mradi huo kunaonesha mafanikio makubwa ambayo tayari yameanza kupatikana
kupitia shughuli za kilimo zinazoendeshwa na wananchi” amesema Dkt. Jafo.
Waziri Jafo
amesema wanufaika wa mradi huo hawana budi kulinda miundombinu ya mradi kwani
ni jambo la msingi katika kuhakikisha hakuna shughuli nyingine za kibinadamu
zitazofanyika katika eneo hilo ikiwemo ufugaji kwa kuwa kusababisha kuporomoka
kwa udongo uliopo katika tuta hilo.
“Tuzuie lango
la maji, tufanye kazi vizuri ya kulinda maji ya bahari yasiye kuchanganyika na
maji ya eneo la mashamba haya na kusababisha mafuriko ya maji yatakayosabaisha
tuta lililopo eneo hilo kuzidiwa na kusababisha kupasuka na kuleta hasara
ambayo ingeweza kudhibitiwa” amesema Dkt. Jafo.
Kwa upande
wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Dkt. Dkt Omar Shajak
amemhakikishia Waziri Jafo kuwa maelekezo yote aliyatoa kwa Ofisi yake
yatafanyika kazi ili kuhakikisha kuwa mradi huo unaleta tija na manufaa
yaliyokusudiwa.
“Mhe. Waziri
maelekezo yako tumeyasikia, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ndiyo msimamizi
wa masuala ya mazingira hapa Zanzibar na pia katika ziara hii pia nimeongozana
na Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi hii, Bi. Farhia Ali Mbarouk ambaye pia
amesikia maelekezo yako” amesema Dkt. Shajak
Naye Afisa
kutoka Wizara ya Wizara
ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Bw. Mbaraka Mgau
amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Januari 2021 na kukamilika Juni 2021 ambapo
jumla ya wakulima 271 wa Shehia ya kiongoni katika Bonde la Tovuni wananufaika kupitia
mradi huo.
Akifafanua
zaidi Bw. Mgau amesema kabla ya kuanzishwa kwa mradi katika eneo hilo lenye
ukubwa wa ekari 6 mazingira ya eneo hilo la mashamba liliathirika kwa kiasi
kikubwa na maji ya bahari ambayo yaliingia kwa kasi kubwa katika mashamba ya
wananchi na hatua iliyorudisha nyuma juhudi za uzalishaji wa mazao ya wakulima
ikiwemo kilimo cha mpunga.
“Huu ni msimu
wa pili wa mavuno tangu mradi huu uanzishwe, ambapo kiwango cha mavuno ya zao
la mpunga kimeongezeka kutoka tani moja hadi tani moja na nusu. Tunashukuru
Kamati iliyoundwa na wakulima wa Shehia hii kwa kutupatia ushirikiano mkubwa
katika kutekeleza mradi” amesema Mgau.
No comments:
Post a Comment