Habari za Punde

WAZIRI DKT. CHANA ATETA NA BALOZI WA UFARANSA HAPA NCHINI MHE. NABIL

 

Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Bolozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlioui  mazungumzo hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Julai 12, 2023 Jijini Dar es Salaam, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui.

Mazungumzo yao yalikua na lengo la kushirikiana baina ya Nchi hizo mbili katika Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambapo Ufaransa kupitia Balozi huyo,  ipo tayari kuleta Wataalam wa michezo mwezi Septemba mwaka 2023 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa hapa nchini.

Mhe. Chana amewakaribisha katika Chuo Cha Michezo Malya na Butimba ambapo kuna wanafunzi wanaosoma michezo.

Mhe. Chana ameongeza kuwa Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Ufaransa imeanzisha Kituo cha kujifunza lugha ya Kiswahili.

Kwa upande wa Balozi Nabil Hajlaoui amesema nchi yake inaendelea kukuza Lugha ya Kiswahili ambapo  amesema nchi hiyo ipo tayari  kuunga mkono ujenzi wa Shule  Kiswahili hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.