Habari za Punde

DOKTA NCHEMBA ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA HUWAEI BEIJING

Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na ujumbe wake wakiangalia mfano wa gari (Fibre Optical Car) lililowekwa mifumo ya kuzuia makosa ya usalama barabarani ikiwemo kutambua madereva wanaendesha vyombo vya moto huku kuongea na simu, waliotumia kilevi na mfumi huo kutuma taarifa zao kwenye mifumo ya kudhibiti matukio ya usalama barabarani, alipotembelea Kampuni ya Huawei, Tawi la Beijing, China, ambapo pia walijadili uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania

Na Benny Mwaipaja, Beijing

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwiguu Lameck Nchemba, ametoa wito kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei ya China, kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kisasa ya teknolojia ya Mawasiliano itakayowezesha nchi kuboresha ukusanyaji mapato yake ya ndani na kupunguza malalamiko ya watumiaji wa mifumo hiyo wakiwemo wafanyabiashara.

Dkt. Nchemba ametoa Rai hiyo Beijing nchini China alipoongoza Ujumbe wa Tanzania kutembelea Kampuni hiyo Tawi la Beijing ambapo masuala kadhaa ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania, yalijadiliwa.

Alisema kuwa mifumo iliyopo nchini ya kukusanya mapato ya ndani ya Serikali haisomani (haiwasiliani ipasavyo) na kuzua malalamiko kutoka kwa watumiaji lakini pia hali hiyo inaikosesha Serikali mapato.

Dkt. Nchemba aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu Elimaamry Mwamba, Balozi wa Tazania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Viongozi wengine wakuu wa Taasisi za Serikali ikiwemo Tanroads na Shirika la Reli Tanzania TRC, alisema kuwa ujumbe wa Tanzania umejionea mageuzi makubwa ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano TEHAM iliyobuniwa na Kampuni hiyo.

Alisema kuwa miaka michache iliyopita Kampuni hiyo ilikuwa ni ya kawaidia lakini baada ya kuwekeza kwenye utafiti wa tenolojia janja, Huawei imekuwa Kamouni kubwa na inayoheshimika ulimwenguni na kwamba inaweza kuisaidia Tanzania kuboresha mifumo yake ya ukusanyaji mapato yake kwa njia ya kodi mbalimbali.

Aidha, Dt. Nchemba ameuomba uongozi wa Kampuni hiyo ambao uliongozwa na Makamu wake wa Rais Bw. Zhang kwenye mazungumzo hayo, kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania za kuongeza ujuzi wa masuala ya TEHAMA kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwenye Kampuni hiyo ili nchi iwe na vijana wabobezi kwenye masuala ya mawasiliani hivo kukuza ajira na kujiongezea kipato.

Aliiomba pia Kampuni hiyo kuwekeza nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu janja ili wananchi hususan waishio vijijini wapate simu janja kwa bei nafuu na ziwasaidie katika kazi zao za kujipatia kipato na kwamba soko kubwa la ndani ya nchi na nchi jirani ni kivutio kikubwa cha uwekezaji huo.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa HUWAEI Bw, Zhang, Meneja wa Huawei Tawi la Tanzania Bw. Russel Zhao, alisema kuwa Kampuni yake imepokea mamobi ya Serikali kupitia kwa Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na kwamba itaangaza fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania na kuwekeza mitaji na teknolojia.

Alisema kuwa uhusiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati ya China na Tanzania unaendelea kuleta hamasa na kwamba Kampuni hiyo itaangalia uwezekano wa kurejesha Ofsi yake Tanzania kwa hivi sasa wanafanya shughuli zao nchini Tanzania kutokea nchi Jirani ya Kenya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.