Habari za Punde

Mhe Hemed aendelea na ziara yake ya kuangalia uhai wa chama jimbo la Mtambwe kisiwani Pemba

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Mtambwe Kaskazini akiw akatika ziara yake ya kuimarisha Chama Jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipokea Vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia Maskani ya CCM Mtambwe Kaskazini Jimbo la Mtambwe vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Pemba Maida Hamad Abdallah.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla, Viongozi mbali mbali na wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii mara baada ya zoezi la kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliojiunga CCM wakati wa ziara ya kuimarisha Chama Jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema kuna kila sababu ya Jimbo la Mtambwe kubaki katika Ngome ya Chama cha Mapinduzi katika ngazi zote za Uongozi ifikapo Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 

Akizungumza na wana CCM na wananchi wa Jimbo la Mtambwe huko katika viwanja vya kisiwani Mhe. Hemed amesema Chama kinahitaji kuimarishwa na kusimamiwa vizuri katika Jimbo hilo kwa kuongeza nguvu za kuwashawishi wananchi wa Mtambwe ili waweze kuendelea kujiunga kwa wingi na CCM.

 

Ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kina dhima kwa wazanzibari kuwatumukia kupitia ahadi walizoweka kama maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi inavyoeleza ambapo SMZ chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi itatatua changamoto zote zinazowakabili wazanzibari.

 

Amewataka Viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuendelea kutangaza mazuri yanayofanywa na Chama cha Mapinduzi na kuachana na siasa za chuki na uhasama badala yake washirikiane katika kuinadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuitekeleza kwa vitendo jambo ambalo litatoa wigo mkubwa kwa wananchi wa mtambwe hususan wapinzani wavutiwe na hatimae kujiunga na CCM.

 

Amewataka Viongozi kuwa na uzalendo wa Nchi yao kwa kuipigania na kuitetea Nchi yao sambamba na kujipanga katika kushinda kwa kishindo katika Jimbo laTambwe na Majimbo yotess ya Zanzibar.

 

Amesema ili kuleta mabadiliko majimboni ni lazima Viongozi kuwa wabunifu katika kuunda miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itawapatia vijana kujiajiri na kuwaweka pamoja katika kukiimarisha chama.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Mberwa Hamad Mberwa ameeleza Mjumbe huyo wa Kamati Kuu kuwa Kamati ya Siasa Mkoa na Wilaya zitahakikisha zinasimamia maelekezo aliyoyatoa na kuyafanyia kazi kwa ngazi zote kuanzia Mkoa hadi Shina

 

Amemuhakikishia kuwa Mkoa wa Kaskazini Pemba utakuwa ni wa mfano kwa kura nyingi za CCM ukifika Uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025 kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Majimbo yote ya Mkoa huo.

 

Muwakilishi wa Jimbo la Micheweni na Waziri wa Kilimo Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis ameeleza kuwa Serikali imejenga masoko kila Mkoa ili kurahisisha uuzaji wa biashara zinazotoka mashambani kwa ubora na kwa bei za uhalisia. ss

 

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazi Pemba Salama Mbarouk Khatib amempongeza Mhe.Hemed kwa uamuzi wake wa kufanya ziara ya kukiimarisha chama ambapo wanaamini matunda ya ziara hiyo yataonekana kwani mabadiliko makubwa yenye tija yatatapatikana ndani ya chama cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla.

 

Ameeleza kuwa wataendelea kufanya ziara mara kwa mara ili kuhakikisha CCM inajengeka na kuendelea kuwa imara na kuingiza wanachama wengi watakaokuja kukipatia Chama hicho ushindi ifikapo mwaka 2025

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.