Habari za Punde

Mkutano wa maafisa habari wafanyika Zanzibar

Baadhi ya Maafisa Habari waliohudhuria Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Hassan Khatibu Hassan akitoa maelezo  kuhusiana na Ziara ya Maafisa Habari iliofanyika Dodoma katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Afisa Habari Wilaya ya Mjini Msangu Saidi akitoa Mchango wake katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Afisa Uhusiano Mkoa wa Kaskazini Shaame Siami kitoa Mchango wake katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Zanzibar Leo Ali Haji Mwadini akizungumza katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Afisa Habari wa ZRA Makame Khamis akitoa Taarifa ya Jumuia ya Maafisa Habari wa Serikali katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar

Mkurugenzi Habari na Matukio wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Salum Ramadhan Abdalla akitoa hotuba katika Mkutano wa Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR 

Na Rahima Mohamed, Sheha Sheha   Maelezo       1

Maafisa habari wametakiwa kutumia vyombo vya habari vya serikali kutoa taarifa za utekelezaji katika  taasisi zao kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari na Matukio kutoka shirika la Utangazaji Zanzibar Salum Ramadhan kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo katika mkutano wa maafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa taasisi za Serikali huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.

Amesema maafisa kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi wa taasisi za umma kutumia vyombo vya habari ili wananchi wajue maendeleo yanayofanywa na serikali yao.

Aidha amesema maafisa habari wanatakiwa kutumia njia mbalimbali kutoa taarifa  katika taasisi zao ikiwemo kuandaa Makala, matangazo  na vipindi mbali mbali vinazotoa uchambuzi  zinazoeleza maendeleo ya nchi.

Vilevile, amewashajihisha maafisa habari hao  kuvitumia vipindi vya asubuhi njema na dira vinavyoendeshwa na shirika hilo ambavyo vinatoa nafasi kwaviongozi wa taasisi mbali mbali kuzungumza na Wananchi.

Mkurugenzi Salum ameipongeza Idara ya habari Maelezo  kwa  kusimamia sera ya habari  na kuwakutanisha pamoja  maafisa hao kwa lengo la kujua maendeleo wanayoyafanya na changamoto wanazokumbana nazo katika majukumu yao ya kila siku.

 

Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo amewataka wakuu wa taasisi mbalimbali kuwashirkisha maafisa Habari katika kazi zao ili jamii iweze kuhabarika juu ya kazi hizo.

 Aidha amewataka maafisa habari kuwa wabunifu  katika kuandaa kazi zao za kihabari na kuendana na kasi teknolojia ya habari na mawasiliano.

 

Kwa upande wao maafisa habari kutoka taasisi mbali mbali, wamesema kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zinarejesha nyuma majukumu yao ipasavyo ikiwemo ufinyu wa bajeti na ushirikishwaji mdogo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.