Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani pamoja na wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023. Mhe. Rais Samia aliwaandalia Madaktari hao wanaotoa huduma ya upasuaji katika Hospitali ya Selian Lutheran Mkoani Arusha Chakula cha mchana kuwashukuru kwa moyo wao wa kujitolea kuwasaidia Watanzania katika sekta hiyo ya Afya
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla
ya Chakula cha mchana aliyowaandalia kuwashukuru na kuwapongeza Madaktari
Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani pamoja na wale wa Tanzania,
Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023.
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Operation Walk USA Paul Gilbert akizungumza kwenye hafla ya Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwashukuru na kuwapongeza Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani pamoja na wale wa Tanzania, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023.
Waziri
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kwenye hafla ya Chakula cha mchana kilichoandaliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwashukuru
na kuwapongeza Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani
pamoja na wale wa Tanzania, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti,
2023.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha
ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Mifupa kutoka California nchini Marekani,
Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Agosti, 2023.
No comments:
Post a Comment