Habari za Punde

Uhamasishaji wa Kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya Zanzibar Waendelea

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa huduma za Afya  Zanzibar Yassir Ameir Juma  akizungumza  na maafisa na wapiganaji wa Chuo cha Mafunzo wakati akihamasishaji maafisa hao  kujiunga na  mfuko huo ,huko Makao Makuu ya Chuo hicho  Kilimani Mjini Unguja .


Na Rahma Khamis Maelezo.   Zanzibar  24/8/2023.

Maafisa na Wapiganaji wa Chuo Cha Mafunzo Zanzibar wameuomba Mfuko wa huduma za Afya (ZHSF) kuharakisha malipo katika vituo vitakasvyochaguliwa kutoa huduma ili kuondosha usumbufu unaoweza kujitokeza.


Wakitoa maoni katika kiao cha kuhamasisha kujiunga na Mfuko huo katika chuo cha Mafunzo magereza wamesma kuchelewa kuwasilisha  fedha katika vituo hivyo kwa wakati  kutazorotesha utoaji wa huduma bora vituoni humo.


Aidha walifahamisha kuwa fedha hizo zinazotoka katika mfuko huo ndizo wanazotumia kupata mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi ikiwemo vifaa tiba.


“ikiwa tutakaa kwa muda mrefu hatujaletewa fedha ambazo zitasaidia kununulia vifaa kama madawa na vifaa vyengine wananchi wetu watashindwa kufika katika hospitali zetu na kwenda kutafuta huduma vituo vyengine,”walifafanua  maafisa hao.


Mapema  Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Mfuko huo  Yassir Ameir Juma amewataka wananchi kuondoa  hofu  kwani Mfuko huo unatarajia kuufanya kila jitihada kuhakikisha  hakutakua na malalamiko  katika vituo vyote  juu ya utoaji wa huduma hiyo.


Amesema mfuko huo utakapoanza kutoa huduma hizo kututakua na utaratibu maalumutakaotumika kwa wagonjwa ili kupunguza gharama za matumizi katika mfuko huo.

                                                                                      

Amefahamisha kuwa mfuko  hautoishia zanzibar kama baadhi ya watu wanavyosema  kwani wanaandaa mikakati madhubuti kwakushirikiana na Mfuko wa Bima  ya Afya wa Tanzania kuhakikisha wananchi wote wanapata  huduma  katika  maeneo yao.


Aidha amesema huduma zote za msingi zitakuwepo katika mfuko huo ili kuepusha usumbufu kwa  wagonjwa ambao wanahitaji matibabu.


Akifafanua zaidi  Kaimu amesema matibabu ni msingi wa maisha ya binadamu hivyo mfuko utafanya kila jitihada kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na zauhakika bila ya usumbufu.

 

Aidha amefahamisha kuwa mwananchi endapo ataumwa lazima anzie Kituo cha afya kilicho karibu na endapo  atapata rufaa ndipo ataendelea kwenda hospitali nyengine kwa ajili ya  matibabu zaidi.  

 

"Kama hatutaweka utaratibu maalumu  gharama itakuwa kubwa na ili mfuko uendelee kuwepo lazima utaratibu huo utumiwe kwani unahitaji kulindwa ili ubaki salama" alieleza.

 

Hata hivyo Kaimu amewataka watoa huduma kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa ili kuepusha malalamiko kwa baadhi ya wagonjwa .

Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Khamis Bakari Khamis akizungumza wakati akaimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko huduma za Afya  Afya  Zanzibar Yassir Ameir Juma  kuzungumza na maafisa na wapiganaji wa Chuo hicho juu ya dhana ya mfuko huo, huko Makao Mkuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja.
Naibu Kamishna Chuo cha Mafunzo Hamdu Haji akiuliza swali kwa watendaji wa mfuko wa huduma za Afya  walipofika kuhamasisha maafisa wa Chuo hicho kujiunga na  mfuko huo huko Makao Makuu ya Chuo hicho  Kilimani Mjini Unguja
Maafisa na wapiganaji wa Chuo cha Mafunzo wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya dhana ya mfuko huduma za Afya  Afya yaliyotolewa na Ofisi ya  mfuko huo na Kufanyika Makao makuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja.
Afisa wa Chuo cha Mafunzo Saada Nassor akiuliza suali kwa watendaji wa mfuko wa huduma za Afya  walipofika kuhamasisha maafisa wa Chuo hicho kujiunga na  mfuko huo, huko Makao Makuu ya Chuo hicho  Kilimani Mjini Unguja

                        PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.