Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa
pongezi hizo jijini Dodoma leo Septemba 13, 2023 na kumtaja Rais Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kuwa ni kiongozi wa mfano katika usimamizi wa mazingira
hususan katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Jafo amesema kuwa
kupitia Serikali anayoiongoza Tanzania imejipambanua
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo ni chachu katika
hifadhi ya mazingira.
Alitolea mfano wa
ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambayo itatumia umeme na zaidi ya shilingi trilioni
23 zimetengwea kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo ambao utasaidia kupunguza gesi
joto ambayo inachangia mabadiliko ya tabianchi.
Sambamba na hilo
ametaja pia mradi wa mabasi wa mwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam
umejipambanua, duniani sasa Tanzania imeaminika na kuwekewa mfano katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Uwezaji katika Bwawa
la Umeme la Nyerere ambapo zaidi ya shilingi trilioni 6.5 zimewekezwa ili
kuja kuzalisha megawati 2,115 na miradi hii yote kimataifa inaonekana ni miradi
ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi,“ alisema.
Aidha, Dkt. Jafo
alisema kuwa kazi kubwa ambayo Rais Dkt. Samia ameifanya katika kipindi cha
miaka miwili ya uwekezaji katika Wizara ya kilimo kwa kuongeza bajeti kutoka shilingi
bilioni 294 hadi shilingi bilioni 950 na bajeti ya mwaka 2023/2024 imetengewa shilingi
bilioni 970.
No comments:
Post a Comment