Habari za Punde

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja : PSSSF Yagawa Miche kwa Wateja Wake Mbeya

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Jijini Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) Oktoba 6, 2023.

NA K-VIS BLOG, MBEYA

MAADHIMISHO ya wiki ya Huduma kwa Wateja yamefikia kilele leo Oktoba 6, 2023 ambapo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametumia maadhimisho hayo kwa kujumuika pamoja watumishi na wateja (wanachama) na kisha wateja kupewa zawadi ya miche wakapande na kuitunza.

Kimsingi wiki ya Huduma kwa Wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwa watoa huduma na wateja.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inatamka “Ushirikiano kwa Huduma Bora.” ikilenga kuhamasisha ushirikiano baina ya watumishi (watoa huduma) wenyewe, lakini pia ushirikiano na wateja ili hatimaye kila upande ufurahie HUDUMA BORA.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, aliwaongoza watumishi wa Mfuko huo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, yenye makao yake makuu jijini Mbeya, kutoa huduma kwa wateja sanjari na kuwapatia zawadi za miche, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Mfuko wa PSSSF, kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na wateja (wanachama) wa PSSSF waliofika kwenye ofisi za PSSSF jijini humo, ili kupata huduma, Bw. Kijazi alisema, Mfuko unawathamini sana na katika maboresho makubwa ya utoaji huduma, mtumishi anayekaribia kustaafu sasa atawasilisha madai kupitia mtandao.

Pia, PSSSF imewarahisishia wastaafu wake kujihakiki kupitia simu janja (Smart phones).

“Mstaafu akishajihakiki kwa alama za vidole (biometric) hatalazimika tena kuja ofisini kujihakiki, na badala yake atatumia simu janja (smart phone) kujihakiki akiwa mahala popote.” Alifafanua Bw. Kijazi.

Miongoni mwa huduma ambazo Bw. Kijazi alishirikiana na watumishi kuwahudumia wateja (wanachama) ni pamoja na huduma za Uhakiki, huduma za taarifa za michango, lakini pia kusikilzia changamoto kutoka kwa wateja na kupokea maoni kwa nia ya kuboresha zaidi utoaji huduma.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhan Mgaya (kulia), akimkabidhi zawadi ya mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa PSSSF kwenye ofisi za Kanda jijini Mbeya

Mteja akihudumiwa huku akiwa na mche aliozawadiwa na Mfuko.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mfuko wa Pensheni PSSSF Paul Kijazi, (kulia) akimkabidhi mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa Mfuko huo, Kanda Nyanda za Juu Kusini, kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika ofisi za Kanda zilizopo Jijini Mbeya.

Bw. Kijazi (kulia) akimuhakiki mteja (mwanachama) kupitia mashine maalum (Biometric)
Katika kujenga upendo na ushirikiano baina ya Mfuko na wateja (wanachama) Bw. Kijazi akiwapatia keki wateja waliofika PSSF Ofisi ya Mbeya Oktoba 6, 2023.
Katika kujenga upendo na ushirikiano baina ya Mfuko na wateja (wanachama) Bw. Kijazi akiwapatia keki wateja waliofika PSSF Ofisi ya Mbeya Oktoba 6, 2023.
Bw. Kijazi na watumishi wengine wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Mfuko.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (wapili kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Jijini Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) Oktoba 6, 2023.

Wateja wa PSSSF, wakiwa na zawadi zao za miche ya Parachichi waliyopewa baada ya kuhudumiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Mbeya Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (kushoto), akimsikilzia Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhan Mgaya wakai w ahafla hiyo.
Bw. Kijazi na viongozi wengine wa PSSSF, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wa PSSSF, baada ya kuhudumiwa na kupatiwa zawadi ya miche ya Parachichi.
 Bw. Kijazi (katikati) na Meneja wa Kanda, Bw. Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wengine wa Mfuko.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.