Habari za Punde

Mama Maryam Mwinyi amtembelea Mke wa Rais wa Burundi, BujumburaMke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi amemtembelea Mke wa Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia maendeleo Burundi Mhe.Mama Angeline Ndayishimiye katika ofisi zake zilizopo Bujumbura Burundi leo tarehe 12 Oktoba 2023.
Mama Mariam Mwinyi ameshiriki zoezi la upandaji mti kuashiria umoja na mshikamano kati yao wakiwa viongozi wanawake Afrika.
Pia mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake UNWOMEN kikanda - Afrika Awa Ndiaye Seck alishiriki.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.