Habari za Punde

Uzinduzi wa maadhimisho ya PSSSF ya wiki ya kimataifa

 

 

 *Atoa huduma kwa wateja

*Awashukuru watumishi kwa kujiongeza, kutoa ushirikiano na ubunifu

*Akabidhi miche ya miti kwa wateja kuenzi Kampeni ya PSSSF ya upandaji miti

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba amezindua maadhimisho ya PSSSF ya wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja Oktoba 3, 2023, Jijini Dodoma.

Akizindua maadhimisho hayo kwa upande wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba ameungana na watumihi wa Mfuko huo kutoa huduma kwa wateja (wanachama) waliofika kwenye ofisi za PSSSF na kisha kuwapatia zawadi za kumbukumbu ikiwemo miche ya matunda.

Mmoja wa wanachama aliowahudumia na kisha kumkabidhi mche wa mti ni Bi. Hapiness Kusaga.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni na PSSSF ina lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Wakati wa uzinduzi huo, CPA Kashimba amewashukuru watumishi wa PSSSF kwa kufanya kazi kwa bidii, kuimarisha ushirkiano baina yao ambao umechochea kutoa huduma bora; na  ubunifu  wao uliosaidia mabadiliko makubwa kwenye huduma.

CPA Kashimba ametoa hamasa kwa watumishi kuendelea kujituma na ameahidi kutoa motisha kwa watumishi watakaojiongeza na kutoa ushirikiano mzuri. Maadhimisho ya Kimataifa mwaka huu yana kaulimbiu isemayo "Team Service"; inayohimiza ushirikiano wa watendaji wote kwenye utoaji wa huduma maridhawa.

Maadhimisho hayo yameshuhudiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji Mbaruku Magawa, Meneja wa Huduma Laila Maghimbi na watumishi wa Idara ya Huduma kwa Wateja iliyoko Makao Makuu.

PSSSF inaadhimisha wiki hii kwenye Ofisi zake nchi nzima, ambapo imeandaa programu mbalimbali za kuelimisha wanachama kuhusu huduma zake.

Maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Huduma kwa Wateja yanaadhimishwa duniani kote kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kuunga mkono juhudi za watoa huduma  katika kutoa huduma na suluhisho la huduma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA Hosea Kashimba, (katikati), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo, Bi. Happiness Kusaga, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja kwenye makao makuu ya PSSSF, jijini Dodoma Oktoba 3, 2023. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Paul Kijazi, na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Mbaruku Magawa.

CPA. Hosea Kashimba akimkabidhi mche, Bi. Happiness Kusaga baada ya kumuhudumia.












No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.