Habari za Punde

Rais Samia Suluhu Hassan amtembelea Aliyekuwa Mke wa Mfalme wa Qatar Sheikha Moza Bint Nasser Jijini Doha nchini Qatar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa aliyekuwa Mfalme wa Qatar Sheikh Hamad Bin Khalifa Al- Thani, Sheikha Moza Bint Nasser Al-Missned wakati alipomtembelea Jijini Doha nchini Qatar  tarehe 03 Oktoba, 2023. Mazungumzo yao yalilenga zaidi masuala ya Elimu na jitihada za pamoja za kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo kwa sababu mbalimbali. Sheikha Moza pia ni Mwenyekiti wa Wakfu wa Qatar.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.