Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wengine wa Wizara ya Afya alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania.(Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasan,  uliofanyika leo 3-10-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Afisa Masoko wa Hospitali ya Aga Khan Tanzania Rukhsar Kanji , wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali za Afya Tanzania,  kabla ya kuufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliofanyika leo 3-10-2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Rais wa THS Dkt.Omary Chillo, wakimsikiliza Sister Mary Shadrack alipotembelea banda la OR –TAMISEMI Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Lishe, kabla ya kufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliofanyika leo 3-10-2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa Mipango wa Taasisi ya Girl Effect Tanzania.Bi.Rita Moses Mbeba, wakati akitembelea banda hilo katika maonesho ya Taasisi mbalimbali za Afya Tanzania, kabla ya kufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023. na (Kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia na kuufungua mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu)
WASANII wa Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaamu wakitowa burudani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summiti) uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati akiufungua Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu leo 3-10-2023.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kumi (10) wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua mkutano huo, unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 3-10-2023 na (kushoto kwake) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. John Jungu.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.