Habari za Punde

Waziri Mhe.Prof. Mbarawa Ang'aka Kutoridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa SGR Makutopora - Tabora

Waziri wa uchukuzi  Prof.Makame Mbarawa akikagua tuta la reli ya kisasa akiwa na viongozi wa mbalimbali wa shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na mkandarasi Yapi Merkezi.
Mitambo ya Mkandarasi  Kampuni ya Yapi Merikezi ikiwa kazini .
Waziri wa uchukuzi  Prof.Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mkanadari wa reli ya kiksasa kulia na kushoto ni Kaimu mkurungezi mkuu wa TRC ,Mhandisi Senzige Kisenge aliyevaa shati la Bluu. 

Na. Lucas Raphael,Tabora.

Serikali imesema bado  hajiridhishwa na kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Makutupora -  Tabora  huku akimwagiza mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi  huo ili kuendana na muda elekezi wa kimkataba.

 

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa uchukuzi  Prof.Makame Mbarawa   alipokuwa katika  ziara mkoani Tabora  alipokuwa  anakagua mradi huo wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Makutupora  - Tabora  chenye urefu wa kilometa  368 .

 

 ambapo amesema  ujenzi huo  kwa sasa ulikuwa unatakiwa kuwa umefikia asilimia 22 ukilinganisha na sasa upo asilimia 12.

 

Alisema kwamba kufuatia kusua sua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo amemtaka  mkandarasi  anayetekeleza mradi huo kupitia kampuni ya kigeni ya Yapi Merkezi kuongeza kasi ya ujenzi  ili kufidia muda  wa asilimia 10 ambao umepotea  katika utekelezaji wa mradi huo

 

Hata hivyo   alitoa agizo kwa shirika la reli Tanzania  (TRC) kuhakikisha  wanaendelea kusimamia  viwango vya ubora katika mradi huo.

 

Prof. Alisema viongozi wanaosimamia wakijipanga vizuri na kuweka mikakati yao itasaidia kurudisha mpango wao wa kumaliza kwa wakati ujenzi huo.

 

Waziri huyo alisema kwamba bado anaamini kuwa viongozi watasimamia vizuri na mradi utamalizika na changamoto zitakwisha na watasonga mbele.

 

"Changamoto katika ujenzi wa tuta kuna mambo ya msingi nitazungumza na Mkandarasi Yapi Merikezi kuhakikisha mradi unakwenda haraka na watafanyakazi ili ule muda uliopotea utakaa vizuri" alisema

 

Aliwapongeza TRC  kwa kumpa fulsa ya kutembelea mradi huo wa reli ya kisasa SGR kutoka Makutupora hadi Tabora. 

 

Naye Kaimu mkurungezi mkuu wa TRC ,Mhandisi Senzige Kisenge amekiri kuwepo kwa changamoto ya kutoteleza mradi huo kwa wakati kwa sababu ulianza mwezi Machi 8 mwaka 2022 na mkataba kumalizika januari 2026.

 

Alisema kipande cha kwanza Dar-es -salaam hadi Morogoro kilometa 300, imefikia asilimia 98.5 na cha pili  Morogoro - Makutupora kilometa 422 kimefikia asilimia 94 ,Makutupora -Tabota 368 upo asilimia 12.

 

Kwa upande wake Meneja Mradi huo,Mhandisi Edwen Ntahondi alisema ujenziwa SGR  kipande cha tatu una jumla ya kilometa 294 kwa njia kuu na kilometa 74 njia za kupishana .

 

Alisema kwamba Mkataba wa utekelezaji huo ulianza 8 marchi 2022 na muda wa utekelezaji ni miezi 42 na unatarajiwa kukamilika mnamo januari 2026.

 

Alisema kwamba Hadi kufika septemba 2023 maendeleo ya mradi yalikuwa asilimia 12 ikilinganishwa na mpango kazi wa asilimia 22,hivyo mradi ulikuwa nyuma kwa asilimia 10 na Mkandarasi ameelekezwa kufanya mapitio ya mpango kazi wake na kuandaa upya ili kufidia muda uliopotea.

Ujenzi wa reli ya kisasa maarufu kama SGR  kipande cha Makutupora - Tabora unatekelezwa kwa gharama ya zaidi shilingi Trioni 4.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.