Habari za Punde

ZHSF Yaendelea Kutoa Elimu ya Mfuko wa Huduma za Afya

Mkurugenzi uendeshaji na utumishi  ofisi ya makamu wa pili wa Rais Gharib Haji Kombo akiwakarabisha watendaji wa mfuko wa huduma za afya Zanzibar  kutoa elimu kwa wafanyakazi wa ofisi ya makamu wa pili wa rais huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.

Na Takdir  Ali, Maelezo.25/01/2024.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar wametakiwa kuyafanyia kazi Mafunzo wanayopewa ili yaweze kuleta tija na kufikiwa  malengo yaliokusudiwa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Gharib Haji Kombo wakati alipokuwa akifunguwa Mkutano wa utoaji wa Elimu ya Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) kwa Wafanya kazi wa Ofisi hiyo, huko katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini.

Amesema iwapo Mafunzo hayo yatafanyiwa kazi kwa ufanisi yataweza kuondosha malalamiko ya Wanachama sambamba na kuwa Mabalozi wazuri kwa wenzao.

Amefahamisha kuwa gharama za matibabu zimepanda kwa kiasi kikubwa hivyo ZHSF itasaidia kupunguza ukali wa maisha sambamba na kuwaomba kushirikiana  katika kuimarisha Mfuko huo ili uweze kutoa huduma kwa Watu wote.

Akitoa maelezo katika Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Fedha Mipango na uwekezaji mfuko wa huduma za Afya Khalifa Muumin Hilal amesema Mfuko huo ni wa Wazanzibari wote hivyo washirikiane kwa kuulinda na kuepuka kufanya udanganyifu ili uweze kuimarika zaidi jambo ambalo litafikia malengo ya kutoa huduma kwa Watu waote.

Hata hivyo amewataka Wafanyakazi wa Serikali ambao hawajajiunga na mfuko huo kujiunga ili waweze kupata matibabu katika hospitali za Serikali na Binafsi.

Nao Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar ameomba kufanya uhakiki kwa haraka ili  Wategemezi wao wapate huduma bora za matibabu.

Aidha wameuomba Mfuko kusimamia vituo vya afya kwani kuna baadhi ya Madaktari wanafanya kazi ambazo hawana utaalamu nao jambo ambalo linasababisha athari kwa Wananchi.
Kaimu mkurugenzi fedha mipango na uwekezaji mfuko wa huduma za afya Khalifa Muumin Hilal akichangia mada katika mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa Ofisi ya makamu wa pili wa rais na idara zake juu ya dhana ya mfuko wa huduma za afya  huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.
Afisa uhusiano na masoko  ZHSF Asha Kassim Biwi akitoa elimu ya mfuko wa huduma za afya kwa watendaji wa ofisi ya makamu wa pili wa rais huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.
Afisa mwandamizi uratibu ofisi ya makamu wa pili wa Rais Khamis Akhui Khamis  akiuliza suali kuhusiana na watendaji wa ofisi hiyo walioko Tanzaniabara kuweza kunufaika na mfuko wa huduma za afya wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko huo huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.
Afisa kutoka Ofisi ya makamu wa pili wa Rais  Sleyyum Abdalla Juma akishauri jambo juu ya mfuko wa huduma za afya wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko huo huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.
Afisa kutoka kamisheni ya kukabiliana na  maafa Nachoum Ngwali Haji akichangia katika mafunzo ya kuwajengea uelewa watendaji wa Ofisi ya makamu wa pili wa Rais na idara zake   juu ya dhana ya mfuko wa huduma za afya huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.

Baadhi ya watendaji wa ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar na Ifdara zake wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya dhana ya mfuko wa huduma za afya huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajun Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.