Habari za Punde

ZHSF Yaendeleza Kutoa Elimu ya Mfuko wa Huduma za Afya kwa Wanachama Wake

Kaimu mkurugenzi mkuu mfuko wa huduma za Afya ZHSF Yaasin  Ameir Juma  akitoa elimu  ya mfuko huo kwa maafisa wa idara ya ustawi wa jamii huko sebleni Mjini Unguja.

 

Kaimu Mkurugenz Mkuu wa Mfuko wa huduma za afya Zanzibar (ZHSF) Yaasin Ameir Juma amewataka Wanachama wa Mfuo huo,kufuata tattibu na Sheria zilizowekwa ili kujikinga na matatizo yanaweza kujitokeza.

Ameyasema hayo huko Sebleni Wilaya ya Mjini katika muendelezo wa utoaji wa elimu ya Mfuko huo , kwa Wafanya kazi wa Idara ya maendeleo ya jamii, jinsia , Wanawake na Watoto.


Amesema mtu yoyote atakaechukuwa rufaa bila maelekezo ya Daktari, gharama zitakazojitokeza atagharamia yeye mwenyewe na Serikali haitohusika. 


Amefahamisha kuwa kuna baadhi ya Wateja wanawatolea ukali watoa huduma kwa kuwalazimisha wawape rufaa ya kuenda hospitali wanazitaka wao jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa Sheria.


Amesema ili Mgonjwa apate rufaa lazima kuwe na uthibitisho kutoka wa Dakatari na rufaa hutolewa kwa kesi maalum sio kwa kila mtu anaetaka.


"Jamani kama Watu wote watamiminika katika Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja kutafurika na kusababisha Madaktari kuzidiwa na kushindwa kufanya kazi kwa Ufanisi" alisema Kaimu huyo.


Hata hivyo amesema tayari wameshaanza kupokea malalamiko kutoka kwa Watoa huduma kwamba baadhi ya Wateja wanapopewa maelekezo kurudi katika hospitali za chini wanakuwa wakali na kutolea maneno ya matusi watoa huduma hao.


Hata Hivyo amewataka Wateja hao kuwa na busara kwani Madakatri hao wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na Sheria za Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar.


"Hebu tutizame jamani Daktari ukimtolea maneno machafu ataweza kufanya kazi kwa moyo mkunjufu na kukupa huduma nzuri kama inavyostahiki tubadilikeni wenzangu" alidokeza Mkurugenzi huyo.


Mapema akitoa maelezo katika Mkutano huo Afisa Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Asha Kassim Biwi amewataka Wanachama kujenga imani na Mfuko huo kwani lengo lake ni kutoa afya bora kwa Watu wote.


Hata hivyo amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Watoa huduma kuwa wananchi kulazimishwa kupelekwa hospitali za rufaa jambo ambalo ni kinyume na sheria za Mfuko huo.


Nao Wafanyakazi wa Idara ya maendeleo ya jamii,jinsia, Wanawake na Watoto wameuomba Uongozi wa ZHSF kutoa elimu zaidi kwa wateja wao hadi ngazi ya Shehia ili Wananchi wapate uelewa wa kutosha na kufikia malengo yaliokusudiwa na Serikali.

Afisa masoko na uhusiano ZHSF Asha Kassim Biwi akitoa elimu ya mfuko wa huduma za Afya  kwa watendaji wa idara ya ustawi wa jamii sebleni Mjini Unguja.
Msimamizi mkuu wa wanachama wa mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Ali Idrissa akitoa elimu juu ya dhana ya mfuko huo kwa watendaji wa idara ya ustawi wa jamii huko sebleni Mjini Unguja.
Afisa kutoka idara ya ustawi wa jamii Zanzibar Bakari Silima Faki akichangia wakati wakipatiwa elimu juu ya mfuko wa huduma za Afya huko sebleni Mjini Unguja.
Afisa kutoka idara ya ustawi wa jamii Rehani Haji Sleiman akichangia wakati wakipatiwa elimu ya mfuko wa huduma za Afya huko  sebleni Mjini Unguja.
Afisa kutoka idara ya ustawi wa jamii Zanzibar Salma Lusangi akichangia wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko wa huduma za Afya huko sebleni Mjini Unguja.

Baadhi ya watendaji wa idara ya ustawi wa jamii wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uelewa juuya dhana ya kuanzishwa kwa mfuko wa huduma za afya yaliyoafanyika Sebleni Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.