Habari za Punde

ZHSF Yajadili Robo ya Kwanza ya Mwaka

Kaimu mkurugenzi mkuu mfuko wa huduma za afya Zanzibar ZHSF Yaasin Ameir Juma akifungua kikao kazi cha watoa huduma wa hospitali za Serikali juu ya tathmini ya utoaji wa huduma kwa robo ya kwanza ya mwaka,kilichofanyika michenzani Mall mjini Unguja.
Dkt. Salma Hashoul akichangia katika kikao kazi cha watoa huduma wa hospitali za Serikali juu ya tathmini ya utoaji wa huduma kwa robo ya kwanza ya mwaka,kilichofanyika michenzani Mall mjini Unguja.

Baadhi ya watoa huduma wa hospitali za Serikali wakiwa katika kikao kazi cha kutathmini  utoaji wa huduma kwa robo ya kwanza ya mwaka,kilichofanyika michenzani Mall mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

Na Rahma Khamis, Maelezo Zanzibar. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Yaasin Ameir Juma amewataka Madaktari kuhifadhi taarifa za Wagonjwa wao katika mfumo ili kutunza kumbukumbu na kuondosha usumbufu wakati zinapohitaji.

 

Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa ZSSF Michenzani Mall wakati wa kikao cha tathmini na mrejesho kwa Watoa huduma wa hospitali za Serikali na binafsi juu ya utoaji huduma kwa robo ya mwaka.

 

Amesema kuna baadhi ya Madaktari   wahawaweki kumbukumbu (rikodi)  jambo linaloelekea upotevu wa kumbukumbu na kuleta usumbufu wakati zinaohitajika 

 

Ameeleza kuwa Serikali inachukua jitihafa mbalimbali kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

 

"Tunapoweka kumbukumbu vizuri tutakua tumeisaidia Serikali yetu katika kuimarisha huduma za afya kwa Wananchi wote," alifahamisha Kaimu Mkurugenzi huyo.

 

Aidha amewataka Madaktari kuwapatia dawa Wagonjwa wanaofika Hositali  ili kuwaondeshea usumbufu katika kutafuta  matibabu.

 

"Tujitahidi tujirekebishe tusifanye makosa ili tufikie malengo ya Dkt Hussein Mwinyi katika kuimarisha huduma za afya, alisisitiza Kaimu Yaasin

 

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mimakati maalum kuhakikiaha wananchi wanapata huduma bora za afya ili kuimarisha afya

 

Akizungumzia kuhusu malipo kwa madaktari Kaimu Mkurigenzi amesema wanachama wanachelewa kulipa jambo ambalo ni kinyume kwani sheria ya mfuko inasema malio ndani ya siku 30 uwe tayari umeshalipa.

 

Nae Ahmed Said Kaimu Meneja wa Madai wa ZHSF amesema kuwa lengo  kikao hicho in kukutana na watoa huduma za afya kujadili mambo mbalimbali na  kusikiliza kusikiliza changamoto. 

 

Amesema wanafanya hivyo ili kuwakumbusha kwamba watoe huduma kwa kufuata muongozo wa afya na kuacha mazowea.

 

 Habiba amesema changamoto inayowakabili madaktari wengi ukosefu wa kutumia lugja mbaya kwa wagonjwa.

 

Nao Washiriki wa kikao hicho  wameiomba Serikali kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia Wagonjwa wanaotumia Bima kuzitumia ipasavyo na kuondosha malalamiko yanayoweza kuepukika.

 

Hata hivyo wameumba Mfuko wa ZSHF kutoa Elimu zaidi kwa wananchi kuhusu kuitumia bima hiyo pindi wanaofika hospitali. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.