Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Aongoza Mamia ya Wananchi Uwanja wa Amaan Complex Kutoa Heshima za Mwinsho kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi

GARI Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa limebeba Mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili  Alhajj Ali Hassan Mwinyi likipita katika barabara ya Amani  kuelekea katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kutowa heshima za mwisho kwa Viongozi wa Kitaifa na Wananchi wa Zanzibar.
WAJANE wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan  Mwinyi  Mama Khadija Mwinyi  na (kulia ) Mama Siti Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kuagwa na kutowa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan, hafla hiyo iliyofanyika 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan  na Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi . Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi wakitowa heshima za mwisho kwa Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania,  hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya New Amaan Complex Amaan Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi  Ndaitwah, baada ya kumaliza kutowa heshima za mwisho kwa Hayati Rais wa Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj  Ali Hassan Mwinyi, hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex  Zanzibar.

VIONGOZI Wastaafu wakitowa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.

VIONGOZI wa Dini Zanzibar wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar kwa ajili ya Sala ya Jeneza iliyofanyika katika Masjid hiyo 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Sala ya jeneza ya kumsalia Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi mbalimbali baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza  ya Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu wa Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi, wakati maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 2-3-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Hayati  Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi.,ikisomwa na Mwenyekiti wa Baraza la Fatua Kenya Sheikh.Said Ahmad Ahmad   Badawiwi, baada ya kumalizika kwa maziko ya Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, yaliyofanyika katika Kijiji cha Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 2-3-2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.