Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Ameongoza Wananchi wa Zanzibar Katika Maziko ya Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil Kijijini Kwao Muyuni C Mkoa wa Kusini Unguja leo 9-4-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akibeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil,katika Msikiti wa Mpendae kwa ajili ya Ibada ya Sala ya Maiti iliyofanyika katika Msikiti huo leo 9-4-2024 na kuzikwa Kijijini kwa Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Sala ya Maiti, kumsalia Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Marehemu Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo 9-4-2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika kuitikia dua ikisomwa na Msaidizi Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mtoro Dar es Salaam Sheikh. Abdalla Mundhiri, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, kumsalia Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil iliyofanyika katika Msikiti wa Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja leo 9-4-2024,aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini UngujaRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil, aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijiji kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo 9-4-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Ahmada Yahya Abdulwakil, ikisomwa na Katibu Mtendaji wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume (hayupo pichani) na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Alhajj Dkt.Mohammed Said Dimwa na (kulia kwa Rais) Kaka wa Marehemu.Ndg. Hassan Yahya Abdulwakil na Rais wa Zanzibar Mstaafu wac Zanzibar Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein,baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika Kijijini kwao Muyuni C Wilaya ya Kusini Unguja leo 9-4-2024
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.