Habari za Punde

Wabunge na Wawakilishi wa UWT Magharibi Unguja Wakabidhi Vifaa

Na Takdir Ali. Maelezo.   12.04.2024.

Katibu wa Idara ya Itikadi, Uenezia, Siasa na Mafunzo Chama cha Mapinduzi Zanzibar Comred Khamis Mbeto Khamis amewapongeza Wabunge na Wawakilishi wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi Kichama kwa juhudi wanazozichukuwa katika kuimarisha Chama na Jumuiya zake.

Ametoa pongezi hizo huko Kiembesamaki katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Dimani kichama wakati alipokuwa akifunguwa mafunzo na kukabidhi vifaa mbalimbali ikwemo simu kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya Tehama, yalioandaliwa na wabunge na wawakilishi wa viti maalum mkoa wa Magharibi kichama.

Amesema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa, vitawezesha viongozi wa UWT ngazi ya mashina hadi wilaya kuwaingiza Wanachama katika Mfumo wa electronic na kuweza kujuilikana idadi yao halisi.

Aidha amesema Idara yake ipo katika mchakato wa kuandaa mtaala wa mafunzo hivyo mafunzo hayo yameweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ambapo huo kutakuwa na mafunzo mbalimbali ikiwemo matumizi ya Tehama na mifumo mengine.

Hata hivyo amewataka waliopatiwa mafunzo hayo wayatekeleze kwa vitendo ili yaweze kuleta tija kwa maslahi ya Chama na jumuiya zake.

‘‘Simu hizi mulizopewa zikafanye kazi na musiende kuwaachia Watoto kuzichezea, siku mbili tatu baadae zikanoki na mujaja mukadai mumepewa vimeo.’’amesema Katibu Mbeto.

Nao Wabunge na Wawakilishi wa viti maalum Mkoa wa magharibi kichama wamesema lengo la kuandaa mafunzo hayo ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wanachama Wanawake lakini ni wachache waliojisajili katika mfumo.

“Zoezi hilo linatakiwa kufanyika kwa haraka sana kama munavyojuwa tukabiliwa na daftari la kudumu la wapiga kura hivi karibuni na kama munavyojuwa uchaguzi ni nambar , tunataka tuwe na nambari kubwa ya wapiga kura wetu.” Wamesema viongozi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.