Amesema amani na
kuwaunganisha watu kuwa kitu kimoja ni chachu ya kujenga ustawi bora wa jamii
na kukuza uchumi wa nchi.
Alhaj Dk. Mwinyi
ameyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipokutana na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya
Waislamu wa Madhehebu ya Shia, Tanzania ‘TIC’ Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge
na ujumbe alioongozana nao.
Alhaj Dk. Mwinyi
alisema maendeleo ya
nchi hayaji eneo lenye vurugu au vita, yanaboreshwa kwenye utulivu, umoja,
usalama na mshikamano wa watu, pia nia rahisi kuyafikia.
Alisema, hata kama hakuna
maelewani kwa asilimia zote kwani hakuna jamii isiyo na migogoro lakini
isipitilize ikawa tishio kwa amani, walao sehemu kubwa ya jamii iwe na
maelewano ndipo mafanikio yanapatikana.
Pia, aliwashukuru viongozi wa
dini wa madhehebu yote pamoja na wananchi wa kuendelea kuhubiri na kuiombea
nchi amani na mshikamano, vilevile ameendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aendelea
kuidumisha nchi kwenye amani na utulivu uliopo kwa mafanikio makubwa.
Halkadhalika, ameendelea
kuwashukuru viongozi hao wadini wa medhehebu yote kwa kuendelea kuwaombea heri,
amani na mafanikio makuwa viongozi na serikali ili kuendelea kukamilisha vyema
mipango ya sekali kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Naye, Sheikh Jalala amempongeza Rais
Dk. Mwinyi kwa kazi nzuri ya maendeleo kupitia sekta mbalimbali
ikiwemo mafanikio makubwa yaliyofikiwa kwenye huduma za jamii, ikiwemo maji
safi, umeme, elimu na afya, halikadhalika miundombinu ya barabara na
mawasiliano.
Kwa upande wake Msemaji wa
Jumuia hiyo, Yasmin Aloo pia amepongeza mafanikio makubwa ya maendeleo
yaliyofikiwa na awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya
kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.
Jumuiya ya Waislamu wa
Madhehebu ya Shia, Tanzania ‘TIC’, ilisajiliwa tangu mwaka 1992.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment