Habari za Punde

JAMII YAHIMIZWA KUWAHUDUMIA WATOTO WENYE MARADHI YA MIFUPA (SIKO SELL)ZANZIBA

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Abdulgulam Hussein katikati akiwa pamoja na Madaktari na Wananchi katika Maandamano ya Maadhimisho ya Tatu ya Maradhi SIKO SELL ambayo husababishwa na Vinasaba vinavyotoka kwa Baba na Mama yalioandaliwa na Jumuiya ya SICKLE CELL yaliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Zanzibar.

NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO.

Jamii imetakiwa kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga Watoto wanaosumbuliwa na Maradhi ya Siko Seli na kuhimizwa kuwahudumia lpasavyo ili kulinda afya zao.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Abdulghulam Hussein katika Maadhimisho ya Tatu ya Maradhi hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Siko Sell Zanzibar.

Amesema ni haki ya kila Mtoto kupata Malezi mazuri kwa Wazazi wake ikiwemo Afya yake, Elimu na kuhakikisha Mapenzi  mema kwa Jamii.

 amesema Wizara iko tayari kutoa kila Ushirikiano ili kuona Jumuia hio inasonga mbele na kuweza kufika hadi Vijijini ili kutoa Elimu kwa Jamii Nzima.

Aidha Naibu amesema  Elimu ni jambo muhimu kwa kila jambo na kuwahimiza watu kupima Afya zao ili kuweza kujitambua na kuyajua  Maradhi hayo.

amewaasa Wazazi ambao Watoto wao wanasumbuliwa na Maradhi ya Siko Seli kuishi nao Vizuri na kuwapa mapenzi ili kujihisi nao wapo pamoja na Jamii.

Nao Wanajumuiya katika Risala yao wameiomba Serikali kuzidi kuwasaidia Ili waweze kupata Bima ya Afya kwa wale wote ambao hawana na kuwawezesha waweze kwenda Vijijini ,kwa ajili ya kutoa Elimu sahihi ya Maradhi hayo.

Akizungumzia Changamoto wanazo kabiliana nazo Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanaoishi na Ugonjwa wa Siko Seli    Dk Fadia Hashim amesema ni pamoja na Upungufu wa Damu ambapo hupelekea Mgonjwa wa Maradhi haya kuhatarisha maisha.

Kadhalika Kliniki ya Ugonjwa wa Maradhi ya Mifupa ipo katika Hospitali ya Mnazi mmoja tu,kwa Unguja Na Pemba hivyo inawalazimu wagonjwa kutoka maeneo yote kufuata huduma Hospitali ya Mnazi mmoja .

Menyekiti ametoa Shukurani kwa Wizara ya Afya na Uongozi wa Hospitali Mnazi mmoja kwa kutoa huduma kwa Wagonjwa wa Siko Sel ili kuhakikisha wanakua na Afya Njema.

Maradhi ya  Siko Seli   ni ya kurithi yatokanayo na  Vinasaba vinavyotoka kwa Baba na Mama na kupelekea Mtoto kuzaliwa na Maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.