Habari za Punde

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zenj Flava Visiwani Zanzibar Rico Single Afariki Dunia leo

Msanii wa Muziki Rashid Amini Abdallah Maarufu kama Rico Single, amefariki Dunia Asubuhi ya kuamkia Leo Tarehe 7/06/2024,

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Dada yake aitwae Sofia anasema Msanii huyo alianza kuumwa juzi kuharisha na kutapika akapelekwa hospital akapata drip na kurudi nyumban jana Akiwa Afadhali.

Lakini kwa mapenzi ya mwenyezi mungu Alfajir ya leo saa 12 akafariki akiwa nyumbani kwa dada yake Huyo, 

maziko Yanatarajiwa kufanyika Leo saa 10 jioni Msikiti wa Wales kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa makaburi ya Mwanakwerekwe .

M/mungu aipumzishe Roho ya marehemu mahala pema Peponi AMIN.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.