Habari za Punde

kazi ya kusomesha Qur’aan ni kazi tukufu mno yenye malipo makubwa zaidi - Mhe.Pembe

Na Maulid Yussuf MJJWW.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma amesema kazi ya kusomesha Qur’aan  ni kazi tukufu mno  yenye malipo makubwa zaidi na mwenye kufanya kazi hiyi  ndio mtu bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mhe Riziki ameyasema hayo katika Mashindano ya 12 ya Qur'an Tukufu kwa Wanawake watu Wazima kitaifa, yaliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa  Julious Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Amesema ubora huo  umeelezwa wazi na Mtume Muhammad  rehma na amani ziwe juu yake, ambapo pia Mtume Muhammad alisema wenye  kujishughulisha na Qur’an kwa kuisoma, kuisomesha na kuihifadhisha kama wanavyofanya ndugu zetu hawa wa Ummul Muunina Aisha , basi watu hawa wamepata takrima kubwa ya kuwa ni wateule wa Mwenyezi Mungu.

Mhe. Riziki amesema hadithi hizo chache  zinaonesha umuhimu na ubora  wa Quran katika kuisoma, kuisomesha na kuihifadhi   katika maisha ya Duniani na ya Akhera, hivyo waislamu na  kina mama kuendelea  kuisoma na kuihifadhi Qur-an pamoja na  kuchukua bidii za makusudi kuwasomesha waoto majumbani pale tu watakapoanza kufahamu maneno wanayoyatamka.

"Vijana wetu ndio nguvu yetu pindi tukiwapa malezi mema yanayoendana sambamba na kitabu chetu wataweza kuwa wazuri kwa uwezo wa Allah" .

Amesema umri usiwe tatizo au kikwazo kwao cha kushindwa kuhifadhi Qur-aan, kwani katika mashindano hayo wapo kina mama walio na umri zaidi ya miaka 70 na wameweza kuhifadhi Qur.aan na wameshiri na kupata ushindi. 

Mhe Riziki amesema wanapaswa kufahamu kuwa wanawake ndio nguvu kazi ya maadili mema ya Taifa  na ndio rasilimali pekee ya kujenga jamii bora yenye maadili na tabia njema, hivyo Mhe ametumia fursa hiyo kuwaomba  kinamama hao  na waliopo majumbani kuzidisha juhudi zao katika kuwalea vyema watoto na kuwaongoza vyema vijana,  kwenye maadili mema kwani jukumu la kusimamia maadili sio la Serikali tu pekee bali ni la kila mmoja wetu.

"Niwaombe kina mama wenzangu tushirikiane sote kwa pamoja kuchunga na kulinda maadili ya vijana wetu kwani kila leo tumekua tukiskia matukio ya kusikitisha ya udhalilishaji kwa vijana wetu na watendaji wa matukio hayo ni watu wetu wa karibu katika jamii yetu," amesema

"Hii inaonesha sura ya kuwa  jamii yetu bado ina maradhi ya mmomonyoko wa maadili na hakuna tiba ya maradhi hayo isipokua kushikamana na mafunzo na miongozo tunayopatiwa na dini yetu ya kiislamu",  ametanabahisha Mhe. Riziki.

Aidha Mhe Riziki amesmea Serikali zetu zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinafurahishwa kuona wanashirikiana kwa pamoja katika kujenga maadili mema ya jamii,  hivyo amewaombe  kwa pamoja kusimamia kwa sauti moja kukemea matendo maovu yote na kuhamasishana kufanya matendo mazuri mema yaliyohimizwa na dini.

Amesema hivi karibuni umeingia mwaka mpya wa kiislamu ambao ni 1446 Hijriya na kila Muislamu anawajibu na jukumu la kufahamu kuingia na kutoka kwa mwaka huu, hivyo wakiwa katika mwezi wa kwanza wa kiislamu ambao ni Muharram na ni miongoni mwa miezi mitukufu, wanapaswa  tujitahidi kumcha Mwenyezi Mungu na kuhimizana kufanya mema na kuacha maovu ili Mwenyezi Mungu azidi kuleta baraka  zake katika nchi.

Hata hivyo Mhe Riziki ametumia nafasi hiyo  kuishukuru Jumuiya ya Ummul Muuminina aisha Foundation kwa kuandaa mashindano haya, waliofanikisha mashindano haya kwa namna moja ama nyengine, washiriki wa mashindano hayo pamoja na waliohudhuria kushiriki mashindano hayo.

Pia amewanasihi waislamu na jamii kwa ujumla kuendelea kudumisha amani ,umoja mshikamamno na maelewano baina yao ili Taifa lizidi kubaki katika amani na kupiga hatua za kimaendeleo siku zote.

Akisoma Risala ya mashindano hayo Mjumbe wa Taasisi ya Ummul-Muuminina Aisha, Ukhti Aisha Awadhi amesema mashindano hayo ya wanawake watu wazima,  ni ya 12 kufanyika tangu yalipoanzishwa mwaka 2013 ambapo yalianzia kwa juzuu moja tu, na sasa ni mara ya kwanza kuhifadhisha juzuu 30.

Amesema kwa mujibu wa utafiti waluoufanya wamebaini kuwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara, Mkoa wa Dar es salaam kumekuwa na mwamko mkubwa zaidi ya washiriki na kimekuwa na ongezeko la wanaojiandikisha kushiriki mashindano hayo kila mwaka kwa wanawake watu wazima.

Hata hivyo amesema wanakabiliwa na changamoto ya udhamini wa kudumu kwa lengo la kusaidia kuwapa ari washriki wa mashindano hayo na kuyafanya kuwa endelevu.

Mashindano hayo ya Kitaifa yameshirikisha Mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ambapo mshindi wa kwanza juzuu 30 ni bibi Maryam Yunus Ibrahim, kutokea Taasisi ya Ummul Muumina Aisha ya Dar es salaan, ametunukiwa  kiwanja kiwanja chenye thamani ya shilingi milioni na nusu, saruji mifuko 20, matofali 1000, fedha taslim 
Shilingi milioni 1,500,000/- na nyongeza ya zawadi mbalimbali kwa wadau walioguswa na mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.