Naibu
Msajili wa vyama vya siasa Mohammed Ali Ahmed amesema sheria na kanuni za
maadili ya vyama vya siasa zinaendelea
kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka usawa wa kijinsia pamoja na
kukuza uwajibikaji na kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake ili waweza kushiriki
kikamilifu katika siasa na demokrasia
nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa, Afisa sheria Mwandamizi kutoka
ofisi hiyo Abdulrazak Ali kwenye mkutano wa tathmini iliyoangalia vikwazo
vinavyowakwaza wanawake katika kugombea na kushiriki masuala ya kisiasa uliofanyika ukumbi wa ZURA Maisara mjini Unguja, ambao
uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, vyama vya siasa,
Asasi za kiraia, wanaharakati na viongozi wa dini.
Akizitaja
sheria na kanuni zinazoendelea kufanyiwa marekebisho ni pamoja na Political
Parties Act (2019), Political Parties Code of Conduct (CAP.258 R.E.2019),
Regulation of 2019, na Kanuni za maadili ya vyama vya siasa na kanuni nyenginezo,
marekebisho hayo yatakapo kamilika
yanatarajiwa kuondoa unyanyasaji kwa
wanawake katika kushiriki masuala ya kisiasa.
Afisa
sheria mwandamizi, alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia ni jambo lisilopingika,
hivyo ni muhimu kwa vyama vya siasa kuzingatia hilo kwa kuandaa miongozo imara itakayosimamia maadili na kukemea vitendo vya
unyanyasaji dhidi ya wanawake, sambamba na kuunga mkono wanasiasa wanawake,
wagombea, wapiga kura ambao wanaweza kukabili vitisho, vurugu, kashfa na
dhihaka kutokana na jinsia zao katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Mapema
akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto,
Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Dkt Mzuri Issa amesema kumekuwa na malalamiko ya
wanawake kudhalilishwa wakiwa katika haraki za ushiriki wao katika siasa na
hakuna mifumo mizuri ya kuripoti matukio hayo na upatikanaji wa haki
Nae
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia , Wazee, na Watoto Mhe Anna Athanas Paul, amesema Wizara hiyo imeandaa mikakati maalum ikiwemo
kutoa mafunzo, nyenzo na programu za ushauri ili kusaidia wagombea wanawake.
Tathmini
ya vikwazo kwa wanawake katika kushiriki kwenye siasa na demokrasia imefanywa na TAMWA
Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la
Kitaifa la Kidemokrasia (NDI) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Imetolewa na Kitengo cha Habari
TAMWA – Zanzibar.
No comments:
Post a Comment