Habari za Punde

Bakiza na Bakita zina jukumu kubwa la kukuza na kueneza kiswahili duniani.

Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Mh. Tabia Maulid Mwita amesema bakiza na bakita zina jukumu kubwa  la kukuza na kueneza kiswahili duniani.

Ameyasema hayo huko ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salam katika siku ya mwanamke hazina kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani ( MASIKIDU).
amesema taasisi hizo mbili zina mipango endelevu ya kukitangaza na kukieneza kiswahili hasa kwa wanafunzi wanaosomea lugha hiyo na kuwawezesha pamoja na kupatiwa fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, tayari serikali zote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeshatenga bajet ambayo itatatuwa matatizo ikiwemo ukosefu wa walimu.

Aidha ameeleza namna ya kukienzi kiswahili na kuimarisha tamaduni mbalimbali kwa kuweka mikakati maalum na kuzungumza na balozi juu ya kufunguwa maktaba za kiswahili sambamaba na kufanya biashara ya kuuza makamusi na vitabu tofauti vya kiswahili.

Hata hivyo, waziri Tabia ameeleza ili kiswahili kikuwe na kuimarika zaid nchini wameandaa mashindano ya insha kwa wanafunzi wa primary, secondary na hata vyuo vikuu kwa ajili ya  kuandika lugha fasaha na kutanuwa wigo kupitia lugha hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.