Habari za Punde

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua na kugawa ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa kabla ya hafla fupi ya uzinduzi na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa hafla ya uzinduzi na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji  Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzindua na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji  Jijini Dar es Salaam.






 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.