Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Afungua Kituo cha (ZBS) cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Zanzibar

MUONEKANO wa  Kituo  Kipya cha  Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Zanzibar, cha Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) kilichofunguliwa leo 6-8-2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika eneo la Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika viwanja vya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo Kipya cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika leo 6-8-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kukifungua Kituo Kipya cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Zanzibar, (kushoto) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban, ufunguzi huo uliyofanyika leo 6-8-2024 katika  viwanja vya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kukifungua Kituo Kipya cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Zanzibar, Ufunguzi huo uliyofanyika leo 6-8-2024, katika viwanja vya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja



















 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.