Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, HusseinAli Mwinyi amesema kuwepo kwa Benki ya PBZ Tanzania Bara ni daraja muhimu la kuunganisha Muungano kwa Vitendo.
Rais Dk, Mwinyi hatua hiyo inaonesha ni jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotoa Ushirikiano wa masuala ya kifedha kwa Zanzibar.
Rais Dk,Mwnyi ametoa tamko hilo leo tarehe 13 Oktoba alipozindua tawi la Bemki ya Watu wa ZanzibarPBZ, lilo Wilaya ya Nyamagana Mwanza.
Rais Dk, Mwinyi Amefahamisha kuwa PBz ni taasis ya kifedha inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Benki inayovutia Wananchi wengi kutokana na huduma zake na unafuu wa mikopo.
Amefahamisha kuwa kuendelea kufanya vizuri kwa Benki ya hiyo kunatokana na mtaji ilionao unaofikia Trilioni 2.3 na kuwa Benki inayofanya biashara ya zaidi ya Shilingi Trilioni moja na kuwa miongoni mwa Benki saba Bora hapa nchini.
Rais Dk, Mwinyi ameeleza hatua ya PBZ kufungua matawi kunaongeza fursa za kiuchumi kwa Wananchi wa kada tofauti na kuwahimiza wananchi wa Mwanza kuitumia PBZ kutanua wigo wa Biashara zao kupitia mikopo inayotolewa na Benki hiyo
Amewahakikishia wananchi kuwa PBZ ni Benki inayoaminika kutokana na uadilifu wa watendaji wake na usimamizi Bora wa masuala ya kifedha.
Aidha Dk,
Mwinyi ameeleza hatua ya BPz kuendelea kutoa Misaada kwa jamii kunaifanya Benki hiyo kuwa karibu na jamii na kuaminika.
Ameuelezea Udhamini wa PBZ wa ligi kuu ya Zanzibar na michezo mengine pàmoja Misaada katika sekta Elimu ,Afya na Michezo inaonesha jinsi ilivyojipanga kuisaidia jamii na kuitaka kuendelea na Misaada hiyo.
Rais Dk, Mwinyi amewahimiza Wananchi wa Mwanza kuitumia PBZ kwa kufungua akaunti na fursa za mikopo
Waziri wa Nchi ,Afisi ya Rais ,Fedha na Mipango Saada Mkuya Salum amesema BPB inatekeleza sera jumuishi ya Kifedha inayowafanya wananchi kushiriki kikamili kujiinua kiuchumi kupitia taasis za kifedha.
Amefahamisha kuwa PBZ kuendelea kufungua matawi ni utekelezaji wa maelekezo na miongozo inayotolewa na Viongozi Wakuu wa Serikali zote Mbili za Muungano.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Lameck Nchemba ameipongeza PBZ kwa kutanua huduma zake Tanzania Bara na kuahidi kwa Serikali kuziunga mkono.
Aidha amempongeza Rais Dk, Mwinyi kwa juhudi zake za kuleta Maendeleo Zanzibar na kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi za kifedha kutekeleza malengo ya kuwahudumia wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Arafat Haji ufunguzi wa Matawi ya Benki hiyo ni utekelezaji wa mpango mkakati iliojiwekea ya kutanua huduma katika Mikoa tofauti nchini kote.
Ameeleza kuwa Benki hiyo sasa ina mtaji unaofikia shilingi Trilioni 2.3 na Kuwasisitiza wananchi kuaminika Benki hiyo kwa kutumia huduma Bora zinzotolewa kufungua akaunti na fursa za mikopo.
No comments:
Post a Comment