Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema kufanyika kwa tunzo za TRACE Nchini itachangia kuongeza idadi ya Watalii na Kukuza uwekezaji.
Amesema hayo katika hoteli ya The Mora, Matemwe wakati wa utambulisho wa tunzo za TRACE AWARDS zinazotarajiwa kufanyika Zanzibar kwa mwaka 2025.
Amesema ujio wa Tunzo hiyo za Kimataifa utachangia Kukuza Vipaji na kuhamasisha mashirikiano ya wadau wa Tasnia ya Muziki Nchini.
Ameongeza kuwa Tunzo hiyo ni zaidi ya burudani kwani inaweza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Kijamii na kiuchumi hivyo amewataka Vijana kujiandaa kuchangamkia fursa hiyo.
"Hili ni jambo kubwa, ni jambo la kihistoria. Ni heshima kwa Zanzibar na Tanzania Kwa ujumla, baada ya tukio hili tunaongeza kiwango cha watalii wanaokuja Zanzibar".
Kwa upande wake Mtayarishaji kutoka Trace Music Awards Serveb Mosha amesema Tunzo hizo ni Muhimu katika Kuikuza tasnia ya Muziki na kuiendeleza Vipaji kutoka Afrika ambapo Kwa Mwaka 2025 wamedhamiria kuutangaza Mziki wa Bongo fleva Duniani.
Zaidi ya watu 3,000 kutoka Nchi mbali mbali wanatarajiwa kushiriki kwenye Tunzo hizo ambazo ni Mara ya kwanza zitafanyika Zanzibar Febuari 24- 26- 2025.
Tuzo za Trace Awards zilianzishwa kwa mara ya kwanza tarehe 21 Oktoba 2023 kwaajili ya kuutangaza Muziki wa Afrika na Wasanii wa Afrika waliopo ndani na Nje ya Afrika.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza na Waandishi wa Habari mara Baada ya kumaliza Uzinduzi wa Tunzo za Trace Awads Summit hafla ambayo itakusanya Watalii na Wasanii kutoka Sehemu mbalimbali itakayofanyika Tarehe 24 hadi 25 February 2025 katika Hoteli ya THE MORA ilioko Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
No comments:
Post a Comment