Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Amefungua Mkutano wa Majadiliano ya Afya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Afya, Washirika wa maendeleo, wadau na watendaji wa Wizara hio katika ufunguzi wa Mkutano wa majadiliano wa Wadau wa Maendeleo kuhusu Ugharamiaji wa huduma za Afya Zanzibar  uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya kwa kuboresha huduma  za Afya ikiwemo vifaa tiba na kuendelea kuwasomesha wafanya kazi ili kuweza kuwa na wataalamu bingwa na bingwa ubobezi  watakaotoa huduma  bora za Afya kwa wananchi wote wa Mijini na Vijijini.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa Mkutano wa majadiliano wa wadau wa maendeleo kuhusu ugharamiaji wa huduma za Afya Zanzibar kwa lengo la kufikia adhma ya Afya bora kwa wote uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini  Zanzibar.

Amesema kuwa katika kuhakikisha Serikali inatoa huduma bora za Afya kwa waanchi wote imeamua kufanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya Afya ikiwemo kujenga Hospital kumi(10)  kila  wilaya pamoja na kuweza kuweka wataalamu bingwa na bingwa bobezi ili kuimarisha  huduma bora za afya  kwa wananchi wote.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ili kuweza kufikia  adhma ya Afya kwa wote Serikali imeimarisha hali ya upatikanaji wa dawa nchini, upatikanaji wa chakula kwa wagonjwa sambamba na kuongeza wigo wa utoaji wa matibabu kwa wananchi kama vile huduma ya usafishaji wa figo(DIALYSIS) ambapo kabla wananchi  walilazimika kutumia gharama kubwa za matibabu hayo na wengine kupoteza maisha kutokana na kukosa fedha za kugharamia huduma hio.

Mhe. Hemed amesema kuwa  Serikali imeimarisha vifaa vya uchunguzi ikiwemo XRAY, CT-SCAN, MRI, ULTRA SOUND na vifaa mbali mbali vya maabara pamoja na kuboresha vifaa tiba kwa kujengwa mitambo miwili (2) ya Hewa Tiba (OXYGEN PLANTS) katika hospital ya Mkoa wa Mjini Magharibi - Lumumba  ambayo itatumika katika hospital mbali mbali za Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira Bora ya Afya kwa kuajiri wafanyakazi wapya 1,566 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kujenga hospitali za Mkoa, hospital ya Rufaa ya Binguni pamoja na kutoa fursa kwa wafanyakazi wa Afya kujiendeleza kielimi na kuwajengea uwezo madaktari bingwa na binga bobezi kuweza kuleta ilufanisi zaidi katika itoaji huduma za Afya kwa wananchi.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema katika kutatua chamgamoto mbali mbali, Serikali inaendelea kufanya mageuzi katika mfumo wa kugharamia huduma za Afya ikiwemo kuanzisha Mfumo wa Huduma za Afya Zanzibar chini ya Sheria namba 1 ya mwaka 2023 na kupewa jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi wote wanaoishi Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh amesema lengo la kuwepo kwa Mkutano wa ugharamiaji wa huduma za Afya Zanzibar ni kufanya majadiliano ya pamoja kati ya watendaji wa Wizara ya Afya, washirika wa maendeleo na wadau wa Afya ili kupata njia mbadala za kitaalamu ambazo zitaiwezesha Serikali kupitia Wizara ya Afya kuweza kugharamia huduma za matibabu kwa wananchi wote wa zanzibar.

Mhe. Hafidh amesema gharama za huduma  ya  matibabu duniani  zimekuwa zikipanda siku hadi siku jambo linalopelekea wananchi wengi kutomudu kuchangia huduma hio pale inapobidi hivyo Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeona ipo haja ya kukaa pamoja na wadau wa maendeelo ili  kutafuta namna bora itakayosaidia kupunguza changamoto hio  na kuhakikisha  kila Mzanzibari anaweza  kupata huduma bora za matibabu bila ya malipo yoyote.

Aidha Mhe. Hafidh amewashukuru washirika wa maendeleo wakiwemo  Pharm Access, W.H.O na wengineo ambao wamekuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana  na Serikali kupitia Wizara ya Afya katika kuhakikisha inatoa  huduma bora za Afya kwa wananchi wote wa Zanzibar.

Kwa upande wao Pharm Access na W.H.O ambao wamekuwa washirika wakubwa wa maendeleo katika Sekta ya Afya wamesema kufanyika kwa Mkutano huo utakuwa ni chachu ya  upatikanaji wa huduma bora za Afya na zenye usawa kwa wazanzibari wote bila ya malipo.

Wamesema upatikanaji wa huduma bora za Afya unategemea uwepo wa Sera, Mikakati madhubuti, rasilimali watu na rasilimali fedha hasa katika kufikia adhma ya Serikali ya Awamu ya Nane(8) inayolenga kugharamia huduma za matibabu kwa wananchi wake wote.

Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe… 13 / 11 / 2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.