Habari za Punde

MKUTANO WA WAJASIRIA MALI KUJADILI CHANGAMOTO NA FURSA ZA UPATIKANAJI MITAJI KWA WAJASIRIA MALI WAFANYIKA ZANZIBAR.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Sharif Ali Sharif  akitoa hotuba ya ufunguzi katika hafla ya Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Serikali kuhusiana na Changamoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa Vijana Wajasiria mali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara ZNCC Ali Amour akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni rasmi katika hafla ya Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta Binafsi na Serikali kuhusiana na Changamoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa Vijana Wajasiria mali hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Na.Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 21/11/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Kazi, Uchumi  na Uwekezaji Zanzibar Mhe  Sharif Ali Sharif amesema Serikali inaweka mazingira Bora ya biashara ili kuwawezesha  vijana kujiajiri.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege wakati akifungua mkutano Kati ya Sekta Binafsi na Serikali wa kukjadili changammoto na Fursa za Upatikanaji wa Mitaji kwa vijana Wajasiriamali  wa Zanzibar.

Amesema kuwa Biashara ni Uti wa mgongo hivyo ni vyema  vijana kuwa wabunifu na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuweza  kufanikiwa katika maisha yao.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanya biashara Hamad Hamad  amesema kuwa lengo la mkutano huo ni  kubadilishana uzoefu wa kibiashara ili kuongeza ujunzi zaidi.

Amesema kuwa mradi wa Tanzania Imeimarisha Sekta Binafsi ( Filter future  mradi wa vijana kutoka USAD unawawezesha vijana kwani kupitia mradi huo vijana wameweza kufanikiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ali Amour amefahamisha kuwa mradi huo umewasaidia vijana kuwainua kiuchumi kwani umenufaisha Biashara 600 wakiwemo wanawake 318 katika Biashara hizo.

Aidha  vijana 200 wamepatiwa mafunzo ambayo yamewawezesha kuimarisha Biashara zao, kusaini mikataba tisa na kutoa vijana 30 kushiriki katika maonyesho ya Biashara nane nane.

Akielezea fursa zinazopatika Meneja wa miradi ya Kilimo kutoka Milele Foundation. Fatma Khamis  amesema kuwa Milele inafanya kazi katika Sekta tatu ikiwemo sekta ya Elimu ,afya pamoja Uchumi jamii kwani wana miradi ya kuwawezesha wanawake kwa kufanya Biashara ndogo ndogo na kuwapatia elimu ya biashara ili kuwawezesha.

Nae Hashim Iddi Simba kutoka Wakala wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi (ZEEA) amesema kuwa Kuna kiasi kikubwa Cha  fedha za Serikali ambazo bado vijana hawajazifikia na  kuwataka vijana hao  kuzichangamkia fursa hizo ili kuweza kuzifikia.

 Mkutano huo imeandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara kupitia mradi wa ImArisha Sekta Binafsi uliofadhiliwa na USAD

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.