Habari za Punde

Muonekano wa Barabara ya Uzi Ng'ambwa ambayo inatarajiwa kujengwa na Kampuni ya CCECC pamoja na Daraja  lenye Urefu wa Kilomita 8.2.75 na Upana wa mita Saba.

Na Sabiha Khamis Maelezo 19.11.2024

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwatengenezea wananchi miundombinu imara ili kuleta maendeleo Nchini na kuondosha msongamano.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Uzi Ng'ambwa pamoja na daraja la Uzi Waziri wa Wizara hiyo Dk. Khalid Salum Mohamed amesema Serikali ya awamu ya nane imekusudia kutengeneza barabara zote za Unguja na Pemba kwa kiwango cha lami.

Amesema Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko katika kuwajengea wananchi na kuiweka Nchi katika hadhi na haiba nzuri ya maendeleo ambayo itakuwa chachu ya kukuza uchumi wa nchi.

“Lazima anapokuja mtu Zanzibar akutane na sura ile ile anayoisikia kwa barabara nzuri, mahoteli mazuri, watu wazuri wenye mioyo ya ukarimu pamoja na vyakula vizuri” alisema Dk. Khalid.

Amefahamisha kuwa jumla ya shilingi Bilioni 35 zitatumika katika ujenzi wa barabara na daraja ili kuwatengenezea wananchi miundombinu sahihi na kuondoa changamoto iliyokuepo kwa muda mrefu.

Vile vile ameeleza Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 8.72 ambapo daraja lina urefu wa kilomita 2 na upana wa mita 6.5 ambayo inauwezo wa kupitisha gari mbili kwa pamoja zinazopishana, njia ya wanaokwenda kwa miguu pamoja na reli za kuzuia ajali na daraja litakuwa na urefu wa mita nne na nusu kwenda juu.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema kuwa uchumi wa nchi umekuwa hivyo Kijiji cha Uzi kinakwenda kuandika historia mpya ambayo itabadilisha muonekano na mtazamo wa kijiji hicho katika maendeleo. 

Aidha amewaomba wananchi wa Uzi kuwapa ushirikiano katika kipindi chote cha ujenzi huo na kuondoa tofauti ili kuweza kulitumikia taifa kwa pamoja na kuleta maendeleo sahihi kwa wananchi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wameishukuru Serikiali kwa kuwajengea barabara pamoja na daraja jambo ambalo litasaidia katika harakati zao za kiuchumi na kuwaondolea changamoto nyingi zinazowakabili sambamba na kuitaka Serikali kuendelea kuwatazama kwa kuwaletea maendeleo katika kijiji chao.

Ujenzi wa barabara hiyo umezinduliwa rasmin ambapo unatarajiwa kuanza hivi karibuni, kwa hatua ya mwanzo ujenzi wa kambi ya wakandarasi utaanza tarehe 20 Novemba 2024 na unatarajiwa kuchukua miezi 9 hadi kumalizika kwake na Kampuni ya CCECC ndio wajenzi wa barabara na daraja hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Makame Machano haji akitoa taarifa ya kitalamu katika hafla ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Uzi Ng'ambwa yenye Urefu wa  Kilomita 8.2.75 na Upana wa mita Saba itakayo jengwa  Kampuni ya CCECC pamoja na Daraja la juu  hafla iliofanyika Uzi Wilaya ya Kati Zanzibar. 
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Wananchi katika hafla ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Uzi Ng'ambwa yenye Urefu wa  Kilomita 8.2.75 na Upana wa mita Saba itakayo jengwa  Kampuni ya CCECC pamoja na Daraja la juu  hafla iliofanyika Uzi Wilaya ya Kati Zanzibar. 
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dk Khalid Salum Mohamed akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Uzi Ng'ambwa yenye Urefu wa  Kilomita 8.2.75 na Upana wa mita Saba itakayo jengwa  Kampuni ya CCECC pamoja na Daraja la juu  hafla iliofanyika Uzi Wilaya ya Kati Zanzibar. 















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.