Habari za Punde

PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA JAJI KIPNEKA


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akiaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Kinampanda Mkoani Singida.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (wa Kwanza kulia), Mkuu wa Mkoa wa Singida mhe. Halima Dendego (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Mwenda (wa kwanza Kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Singida mjini (wa pili kushoto) wakiweka maua ya heshima katika kaburi la marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa kwenye mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Kinampanda Mkoani Singida tarehe 06 Novemba 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Singida mhe. Halima Dendego wakiweka maua ya heshima katika kaburi la marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa kwenye mazishi yaliyofanyika kijijini kwake Kinampanda Mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida mhe. Hallima Dendego akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika mazishi ya marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa yaliyofanyika nyumbani kwake Kinampanda Mkoani Singida
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akisalimiana na Mama Kipenka mke wa marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa Jaji katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Kinampanda Mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda akitoa salamu za pole kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi mhe. Dkt Mwigulu Chemba katika mazishi ya marehemu Jaji Mstaafu Kipenka Msemembo Mussa yaliyofanyika nyumbani kwake Kinampanda Mkoani Singida

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa  marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa ambaye alikuwa Jaji Msataafu wa Mahakama kuu ya Tanzania na aliyewahi kushika Nyadhifa mbalimbali Serikalini enzi za Uhai wake ikiwemo Katibu Wa Bunge.

Hafla ya Mazishi yamefanyika leo Tarehe 06 November 2024 katika Kijiji cha Kinampanda Kilichopo katika wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Mhe. Pinda ameshiriki Mazishi hayo akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ameeleza kwa masikitiko juu ya kuondokewa na Marehemu. Jaji Kipenka Msemembo Mussa.


Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Wilayani Kinampanda na kuongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati, Dk. Cyprian Hilinti

Akitoa salamu za rambirambi, Naibu Waziri Pinda amesema kuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mhe. Pinda amesema marehemu Jaji Kipenka  alikuwa kiungo muhimu cha Maendeleo kwa Wananchi wa Kinampanda enzi za uhai wake alikuwa akishirikiana vema na Dkt Mwigulu katika Shughuli mbalimbali za Maendeleo.

"Nimesimama hapa kwa niaba ya mhe. Mwigulu ambaye anatoa pole nyingi sana kwa familia na ameindokewa kwa maelezo yake na mtu muhimu ambaye kilikuwa Kiungo cha Maendeleo cha Kinampanda". Amesema Mhe Pinda

Aidha Mhe. Pinda ametoa wito kwa familia ya Jaji Kipenka hasa watoto wa marehemu kuacha kugombania mali zilizokuwa zinamilikiwa na Marehemu Jaji Kipenka kwani Kifanya hivyo kutawaingiza matatizoni zaidi.

"Kikubwa kwenye familia mtulie wakati wa pito hilo katika kukusanya mali za marehemu", Amesema Mhe Pinda

"Nimeona baba ana watoto wanne lakini watoto kokote waliko wasisahau Mwenza wa Marehemu Jaji Kipenka yupo hai". Amesema Mhe Pinda

Marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa alizaliwa tarehe 28, Desemba 1954 ambapo aliugua kwa muda kabla ya kufariki tarehe 2 November 2024.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.