Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipo katika mchakato wa kuipa dhamana kampuni hiyo ya China Harbour Engineering Co. Ltd kujenga Bandari ya Mangapwani, Unguja.
Katika mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi amemhakikishia Bw. Bai Yin Zhan kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, baada ya kukamilisha mchakato wa maridhiano kwa pande zote mbili, SMZ itatoa ushirikiano ili ujenzi wa mradi huo uanze mara moja.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi amekutana na wawakilishi wa kampuni mbalimbali ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza Zanzibar, zikiwemo Fuhai Group, inayojihusisha na masuala ya nishati, mafuta, na gesi; Chery Holding Group Co. Ltd, iliyobobea katika utengenezaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme; na China Sinopharm International, kampuni kubwa inayotengeneza madawa ya binadamu. Mazungumzo hayo yalilenga kuweka misingi ya ushirikiano itakayosaidia kukuza uchumi na kuboresha huduma muhimu kwa wananchi kupitia uwekezaji endelevu.
📅 06 Novemba 2024
📍Shanghai, China.
No comments:
Post a Comment