Na Takdir Ali. Maelezo Zanzibar.
Waandishi wa Habari Nchini wametakiwa kutumia Kalamu zao vizuri kwa kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwepo Idara ya mashirikiano baina ya sekta za umma na sekta binafsi (PPP).
Wito huo umetolewa huko Ofisi za TRA Mayugwani na Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Khamis Suleiman Mwalim (Shibu) katika muendelezo wa kutoa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari ili kuweza kupata uwelewa wa masuala mbalimbali kuhusu Taasisi zilizomo katika Wizara hiyo.
Amesema PPP ina miradi mingi muhimu inayoshirikiana na Taasisi husika lakini bado baadhi ya Wananchi hawajapata uelewa wa kutosha hivyo iwapo Waandishi wa Habari watafanya kazi za kutoa elimu jamii itaweza kupata uelewa wa kutosha.
Aidha amesema PPP inaangalia kufuatilia uwezekeno wa wa kutoa huduma bora, kwa wakati na kugawana mapato kwa mujibu wa Makubaliano na baadae kurudisha kwa Serikali.
Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Idara ya Mashirikiano Baiana ya sekta za Umma na Sekta Binafsi (PPP) Bakari Mohamed Salum amesema lengo la kuandaa Mafunzo hayo ni kutoa uelewa kwa Waandishi wa Habari ili waweze kupata ufahamu na kuleta mabadiliko katika jamii.
Amesema Serikali imeunda Idara ya PPP ili kuongeza nguvu na kufanya kazi kwa pamoja na kuweza kuleta ufanisi katika miradi ya maendeleo kwa Wananchi.
Nao Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Zanzibar, wameipongeza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji kwa kuweka Utaratibu wa kukutana na Waandishi ili kuweza kubadilishana Mawazo na kupata uelewa wa mambo yanayohusu Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Aidha Waandishi hao wameahidi kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupata elimu na kufikia malengo yaliokusudiwa na Wizara hiyo.
Hata hivyo Waandishi Wizara na Taasisi nyengine kuiga mfano wa Wizara hiyo ili kuweza kuta uelewa zaidi kwa faida ya Wananchi na Taifa kwa Ujumla
No comments:
Post a Comment