Habari za Punde

Kamishna wa TRA Aipongeza ZIC Kwa Ulipiji wa Kodi

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud kufuatia mwaliko wa Rais huyo yaliyofanyika katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Mogandishu. 

 

Viongozi hao wameelezea kuhusu dhamira yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi kati ya mataifa hayo mawili.

Waziri Kombo yupo nchini Somalia kwa ziara ya kikazi ambapo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya kutia saini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia katika sekta ya Afya, Ulinzi,  Utalii na Ushirikiano wa Jumla.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.