SERIKALI ya
Mapinduzi ya Zanzibar, imesema inakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikubwa
cha Utalii wa kisasa usio na misimu kwa kuwavutia wawekezaji na wageni wengi.
Imesema
Zanzibar bado inawakaribisha wawekezaji zaidi kwani ina maeneo mengi ambayo
hayajafikiwa kwa kwa fursa nyingi za uwekezaji.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasea hayo
Ikulu – Zanzibar alipozungumza na Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.
Marianne Young alikuja
kujitambulisha.
Dk. Mwinyi
amesema bado ina Zanzibar ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji kwenye sekta ya Uchumi
wa Buluu kupitia Utalii, Bandari, Mafuta na gesi pamoja na sekta ya
usafirishaji wa majini.
Ameeleza kwa
muda mrefu Zanzibar imekua ikitangaza Utalii wa zamani wa Urithi ukiwemo wa Mji
Mkongwe wa Zanzibar na Fukwe, ameongeza kuwa wakati umefika Zanzibar sasa
kuendelea kujitangaza pia na utalii wa kisasa ukiwemo utalii wa mikutano ya
kimataifa, michezo, akitolea mfano michezo ya mbio za magari ambao umekua
kivutio kikubwa duniani na kuwavutia mashabiki na wageni wengi maarufu kama
(Formula one).
Aidha, Rais
Dk. Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ni kuwa na Utalii wa hadhi ya juu
utakaowavutia wageni wengi kuja nchini bila kujali misimu ya utalii, pia
amesema nchi imejiandaa kuwa na misimu yote ya Utalii kwa kuimarisha vivutio
zaidi vyenye kuwavutia wageni wengi.
Kuhusu
ongezeko la Utalii Dk. Mwinyi ameeleza dhamira ya Serikali kuendelea kuimarisha
miundombinu ya barabara na mawasiliano ikiwemo viwanja vya ndege vya Unguja na
Pemba kuemdelea kuwa na hadi ya kimataifa.
Akizungumzia
masuala ya Uchumi na Uwekezaji Rais Dk.
Mwinyi amesema Bado kuna maeneo mengi ya Uchumi ambayo wawekezaji wakija
wanaweza kushirikiana na Serikali kuyaendeleza.
Kuhusu
Bandari, Dk. Mwinyi amezizungumzia fursa za Bandari jumuishi kwa Zanzibar ambayo
Serikali imewekeza nguvu kubwa huko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja
alikoeleza kwa sasa Zanzibar inahitaji Bandari kubwa ili kukidhi mahitaji ya
uchumi wake kama kituo muhimu cha usafirishaji, usambazaji wa bidhaa, kutoa
huduma na kufanyia biashara ikiwemo kupokelea mizigo, kusafirishia mazao, na
mahitaji mbalimbali ikiwemo mafuta, nafaka, na kukuza uchumi wake.
Kwa upande
mwengine Rais Dk. Mwinyi aligusia suala la mafuta na gesi pamoja na sekta ya
usafirishaji wa majini, akieleza Zanzibar inavyohitaji uwekezaji mkubwa kwenye
sekta hiyo na kuiomba Serikali ya Uengereza kuangalia uwezekano wa kuungamkono
kwenye sekta hiyo kuimarisha sekta ya biashara na uchumi wa Zanzibar kupitia
bandari zake za Uguja na Pemba.
Dk. Mwinyi
pia aligusia eneo la nishati na kumueleza mgeni wake huyo kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inadhamiria kuwa na umeme wa ukahkika kwa kuwa na umeme mbadala
kwa ajili ya wawekezaji waliopo, hivyo, ameiomba Serikali ya Uingereza
kuangaliua uwezekano wa kuweka nguvu zake kwenye eneo hilo.
Hata hivyo,
Rais Dk. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji zaidi wa Uingereza kuja Zanzibar kwa
wingi kuwekeza na kunufaika na fursa za uwekezaji zilizopo.
Akizungumzia
ukulima wa mwani, Dk. Mwinyi amemueleza balozi huyo kwamba Zanzibar inauza zao
hilo kama malighafi kiasi ya kuwa halileti tija kwa Uchumi wa taifa na wakulima
kwa ujumla, hivyo aliwashawishi wawekezaji kutoka Uingereza waje nchini
waanzishe viwanda vya kuusarifu mwani na kuzalisha bidhaa za zao hilo jambo
ambalo litawaongezea tija wakulima wa zao hilo nchini na bidhaa
wanazozizalisha.
Pia
amewaalika wawekazaji wa sekta binafsi wa Uingereza kuitembelea Zanzibar
kubaini uzuri na fursa zilizopo.
Wakati huo
huo, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa ushirikiano wa
diplomasia uliopo baina yao na Tanzania ikiwemo Zanzibar pia kwa kuisaidia Zanzibar
kwa sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na masuala mengine ya jamii.
Naye Balozi Marianne Young amemuhakikishia
Rais Dk. Mwinyi kuwa Serikali ya Uingereza itaendelea kuunga mkono Zanzibar
kuimarisha ustawi wa kuleta maendeleo hasa kwa masuala ya afya, elimu na Uchumi
wa Buluu.
Amesema,
Utalii ni fursa muhimu baina Zanzibar na Uingereza katika kuimarisha
ushirikiano wa pande mbili hizo na kuiahidi Zanzibar kushirikiana kiufundi kwa uzoefu
kwa masuala mbalimbali ya Uchumi, jamii na teknolojia.
Pia Balozi Young alisifu juhudi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa maendeleo makubwa iliyofikiwa hasa kwa sekta ya
mawasilino na miundombinu.
Alieleza
Imani yake ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao na kuahidi uuendeleza kwa
vitendo na utekelezaji katika kuyafikia malengo baina ya pandembili hizo.
Balozi Marianne Young amechaguliwa wadhifa
huo kuhudumu Tanzania mwezi Ogasti mwaka huu.
IDARA YA
MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment