Habari za Punde

DKT. Nchemba Amekutana na Kuzungumza na Rais wa Benki ya Dunia Mhe.Jay Banga

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akisalimiana na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza tarehe 27 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unaotarajiwa kutamatika tarehe 28 Januari 2025 utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.