Habari za Punde

Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi Amefunga Mafunzo ya Pili ya Usimamizi wa Ndao Yaliyofanyika katika Masjid Jamii Zinjibar Mazizini Jijini Zanzibar

Mufti Mkuu wa  Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza katika ufungaji wa Mahafali ya  Pili ya Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa yaliyofanyika katika katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.

Na.Ali Issa -Idara ya Maelezo Zanzibar.

Mufti Mkuu wa  Zanzibar Shekhe Saleh Omar Kab amewata wasimamizi  wa ndoa  kuwafungisha ndoa wanandoa kwa kufuata sheria za dini ya kiislam.

Ameyasema hayo huko Msikiti wa Jamii Zinjibari Mazizini Mkoa wa0 Mjini Magharibi unguja katika  Mahfali ya Wasimamizi wa ndoa mkupuo wa pili.

Amesema kumekuwa na migogoro mingi  ya wanandoa katika jamii inayosababishwa  na baadhi ya wasimamizi wa ndoa kufungisha ndoa  bila ya  kufuata taratibu na sheria za ndoa.

Aidha amesema wapo baadhi ya  watu waliolewa ikiwa mawalii wao sio sahihi  kisheria na baadhi ya wanawake kujiandikia talaka wenyewe jambo ambalo halikubaliki kisheria na hupelekea migogoro katika jamii.

Amefahamisha kuwa msimamizi wa ndoa ni lazima atizame talaka vyeti vya ndoa kwa umakini na aridhike kwani baadhi ya watu hujaribu kufoji talaka na kukosesha haki kwa mume,mke na watoto.

"tutambue kuwa amana ni kitu muhimu utapo mfungisha ndoa mtu bila kufuata taratibu za kisheria utabue kuwa umepoteza mfumo mzima wa ndoa na haki za watu ikiwemo kizazi"alisema mufti Mkuu Seleh Omar Kabi.

Nae Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Khalid Ali Mfaume amesema Ofisi hiyo imekua ikitoa Mafunzo kwa awamu na kwa utaratibu maalum, Ili kupunguza migogoro ya ndoa katika jamii.

Aidha amesema mafunzo hayo yanahusisha sekta mbalimbali  ni pamoja na  wasimamizi wa ndoa kwa mashekhe,Mafunzo ya wanandoa,na Mafunzo kwa walio silimu kuingia katika uislamu.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanaishukuru ofisi hiyo kwa kuwapatia Mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa utaratibu wa Elimu walioipata.

 Mafunzo hayo yameanza Tarehe 22/ 10/2024  hadi tarehe  8/1/2025 yalioshirikisha wasimamizi wa ndoa 175 waliofaulu 170 naTano wameshindwa kutokana na sababu mbalimbali na mada zilizojadiliwa ni Ndoa,talaka na taratibu za kufunga ndoa raiya wa kigeni.
Mufti Mkuu wa  Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (watatu kulia)akitoa hotuba ya Ufungaji katika hafla ya  Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Wakufunzi waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Divisheni ya Utafiti na Utatuzi wa Migogoro na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Ofisi ya Mufti Sheikh Shaban Salim Humud akizungumza kuhusiana na Migogoro ya Ndoa katika hafla ya  Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Mmoja kati ya Masheikh waliopata Elimu ya Usimamizi wa Ndoa Sheikh Khalfan Abdulla Abdulsatar akisoma risala katika hafla ya  Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Ust,Rajab Makame Ali akizungumza kuhusiana na Urajis wa Ndoa na Talaka katika hafla ya  Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Khalid Ali Mfaume akitoa samu za Ofisi katika hafla ya  Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Masheikh waliopata Elimu ya Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa kwa Miezi Mitatu waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo hayo hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Masheikh waliopata Elimu ya Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa kwa Miezi Mitatu waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo hayo hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.16/01/2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.