Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Azungumza na Umoja wa UWAWAZA Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar (UWAWAZA) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum (kushoto kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika leo 17-2-2025 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar (UWAWAZA) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma, mazungumzo hayo yaliyofanyika leo 17-2-2025 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO ya Kuthamini Juhudi yake katika Kukondoisha Masuala ya Jinsia Zanzibar,akikabidhiwa na Mjumbe wa (UWAWAZA) Mhe. Mwantatu Mbarak Khamis,baada ya kumaliza mazungumzo na Ujumbe wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar (UWAWAZA) mazungumzo hayo yaliyofanyika leo 17-2-2025 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuunga mkono Harakati za Jumuiya ya Wawakilishi Wanawake  (UWAWAZA) za kuwajengea Uwezo Wanawake katika Maendeleo yao kisiasa,Kiuchumi na Kijamii.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Wajumbe wa Jumuiya hiyo waliofika Ikulu kujitambulisha  na Kumpongeza Dkt, Mwinyi.

Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Jumuiya hiyo ni sauti muhimu katika kupigania haki za Wanawake ndani na Nje ya Baraza la Wawakilishi na kuahidi kuendelea  kuiunga Mkono  kuyafikia Malengo  yao.

Ameeleza kufarijika na kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo za  kuimarisha  Ushiriki na kuongeza Idadi ya Wajumbe Wanawake katika Baraza la Wawakilishi  kwani Uzoefu unaonesha  Wanawake wanafanya Vizuri katika Uongozi.

Rais Dkt, Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wanawake Kutosita kugombea nafasi za Uongozi katika  Uchaguzi Ujao ili kuongeza Idadi yao katika Baraza la Wawakilishi. 

Rais Dkt, Mwinyi ametoa Ushauri kwa UWAWAZA kufanya tathmini ya Miaka 22 tangu Kuanzishwa kwake ili kubaini maeneo muhimu yanayohitaji Msukumo wa Serikali  kuwainua Wanawake , Kisiasa , Kiuchumi na kijamii.



Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawakilishi Wanawake  Saada Mkuya Salum amempongeza Dkt, Mwinyi kwa  Mafanikio ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, Masoko , Hospitali na Vituo vya Afya ambavyo  vimekuwa nyenzo  muhimu kwa Ustawi wa Wanawake.





 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.