Habari za Punde

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam kumuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu,  Februari 17, 2025.  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknoloji, Profesa Adolf Mkenda, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary  Kipanga,  Kaimu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi,  na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi   ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania , Profesa Hamisi Dihenga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Februari 17, 2025. Kushoto ni  Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela (kulia)  alipotembelea banda la maonesho la CRDB katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,   Februari 17, 2025.  Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji, Omary Kipanga na kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu, Dkt. Bill Kiwia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu Tanzania, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,   Februari 17, 2025.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa  katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu Tanzania, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,   Februari 17, 2025.   Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Elimu, Sayansi na  Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho hayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele  cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam,   Februari 17, 2025
Baadhi ya washiriki wa Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu wakimsikiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassn kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 17, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.