Habari za Punde

Waziri Dkt.Nchemba Ateta na Mwakilishi Mkaazi wa WFP

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Bw. Ronald Tran Ba Huy, baada ya kukutana  na kufanya mazungumzo, Jijini Dodoma, ambapo wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika kukuza uchumi jumuishi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kushiriki katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga, pamoja ma mambo mengine, kukuza, ajira, kupambana na umasikini, kukuza mauzo ya budhaa nje ya nchi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia za upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.